Ni sawa KVA = Kilo Volt-Ampere, lakini sio sawa na KW (KiloWatts). Kwa machine kama generator (ina resistors, capacitors na inductors), KVA rating yake sio sawa na KW. Katika hali kama hii KVA huwa ni kubwa kidogo kuliko KW. Inabidi KW kugawanya na factor fulani (power factor) ili kupata KVA.
KVA = KW/Power Factor
Kwa kesi yako, KVA = 2.5/Power factor. Hii power factor inategemea tofauti ya 'phase' kati ya current na voltage kwa system husika. Kwa kukadiria huwa inatumika 0.8
Hivyo, utapata: Generator yako iwe angalau 2.5/0.8 = 3.1 KVA. Hivyo ni vizuri ukanunua generator ya kati ya 3.2 - 3.5KVA itakufaa.