Naomba msaada, kanusha sentensi hii "ameshiba sana"

hajashiba sana, ndio sahihi

maana ameshiba sana "me" ni ya wakati uliopo timilifu....

ivyo kusema ajashiba sana dhima ya "Ja" ni kuonyesha njeo ya wakati huo huo uliopo lakini timilifu!!!
 
Hajashiba sana ni kwa wakati uliopo.

Ni jibu la swali "ameshiba sana?"

Hakushiba sana ni kwa wakati uliopita.

Ni jibu la swali "alishiba sana?"
 
Mkuu kinachofanyika hapa ni kitu cha kitaaluma , yaani sarufi maana ( semantikia) kama hujui afadhali upite tu!
katika neno "hajashiba " mofu ( kwa mujibu wa Chomsky et el ) "-ja-" inafanya kazi gani?

ha- hiki no kiambishi awali kinachoonesha nafsi ya tatu umoja, lakini pia huonesha ukaunushi wa tendon yaani kushiba.

-ja- ni wazi kwamba lugha ya kiswahili ina njeo ambazo zinafahamika kama vile -li-, -na-,-me- na -ta- lakini pia tukumbuke pia lugha ina sifa ya kughairi sifa na taratibu ya lugha yenyewe.

Hivyo basi, mofu - ja- inaingia katika njeo ya wakati uliopo hali timirifu..
lakini pia ni kighairi cha lugha.

Hii ni kwasababu nikitaka kuonesha wakati uliopita nitasema "hakushiba"

kana utakubali kuwa "Ku" ni njeo basis hata "ja" itakuwa njeo kwa sababu zina uwezo wa kubadilushana nafasi.

Akhsante.
Jibu la mwanasarufi aliyekomaa.
 
Ameshiba sana=Hajashiba sana
Alishiba sana=Hakushiba sana
Atashiba sana =Hatashiba sana
Anashiba sana =Hashibi sana
 
"Hajashiba sana" kimantiki 'ja' dhima yake ni wakati uliopita kitambo ni sawa na dhima ya 'has' ambayo ndani yake kuna kitu kinaitwa 'participle kwenye sarufi ya kiingereza.' lakini 'ku' ni dhima ya wakati uliopita lakini 'tilifu yaani past perfect'...

Naomba msaada jaman kuna watu tunabishana nao hapa wengine wanadai ''hakushiba sana''kwa madai Kwamba sarufi ya kiswahili haina dhima ya ''Ja''
Na wengine wanadai 'hajashiba sana' lakini wanashidwa kutoa dhima ya 'ja' na 'ku' inaonesha wakati uliopita Kwa wanaounga hajashiba sna
 
Hajala sana.
Naomba msaada jaman kuna watu tunabishana nao hapa wengine wanadai ''hakushiba sana''kwa madai Kwamba sarufi ya kiswahili haina dhima ya ''Ja''
Na wengine wanadai 'hajashiba sana' lakini wanashidwa kutoa dhima ya 'ja' na 'ku' inaonesha wakati uliopita Kwa wanaounga hajashiba sna[/QUOTE
 
mkuu kikanushi lazma kiwe hajashiba
angalia mifano mingine
hajaleta
hajafika
hajaniambia etc. hii inasimama kama kiambishi cha wakati uliopo hali timilifu. na kikanushi ni ha-
 
Back
Top Bottom