bigmind
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 12,457
- 12,668
Jamani hapa, ninajisikia kama kufa kabisa, ijumaa nilienda kuweka kambi kwenye pori moja kwa muda wa siku 2, kulikuwepo na mbu sijapata ona, niling'atwa si kawaida kusema kweli haraka nilijitabiria malaria ile jumapili narudi home nikawa hoi tayari malaria. Sasa nikachukua mseto, hizi dawa za wizara ya Afya.
Shida yangu ni kuwa dawa inanikwatuza tumbo sijapata ona, tumbo linanyonga mpaka nalia...!
Nilianza dozi jumapili usiku saa nne, bado vidonge nane tuu ambavyo vinapaswa kuisha kesho, ila hapa tayari nimeghairi sitavimalizia, je hili tatizo ni kwangu au kila mtu anasumbuliwa na mseto. Msaada jamani nafwaa...