Naomba msaada: Bajeti ya Mkulo itajadiliwa tena? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada: Bajeti ya Mkulo itajadiliwa tena?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mawenzi, Jul 19, 2011.

 1. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Dear Great thinkers!! Budget mama (ya Mkulo) imepitishwa. Ndani yake kuna hii ya Ngeleja iliyokataliwa.

  Ngeleja atatengeneza nyingine ambayo itawakilishwa bungeni, na hii mpya lazima itakuwa tofauti sana na ilyokataliwa (ambayo imo ndani ya ile ya Mkulo). sasa hapa itakuwaje: bajeti mpya ya Ngeleja itaingiaje ndani ya ile ya Mkulo?? Ikiingizwa ndani ya ile ya Mkulo na kuifanya iwe mpya, je ya Mkulo itabidi ipitishwe upya?? Au itakuwaje?? Nielimisheni tafadhali.

  Ahsante sana
   
 2. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Swali maridadi kabisa! Sijajua Kanuni za Kudumu za Bunge zinasemaje kuhusu hili!
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo nawashangaa wabunge wa chama tawala wakati wenzao wa upinzani wakikataa kuwa bajeti haijakabiliana na tatizo la umeme wao walipiga meza na kupayuka Ndiyoooooooooooooooooo. Wenzao wa upinzani walipohoji kodi za mafuta zipunguzwe ili kupunguza mfumuko wa bei wao waliipongeza kwamba hii ni bajeti nzuri sana inayowajali wananchi.

  Leo hii mfumuko wa bei umeendelea kupanda;
  Mafuta ya taa ni kilio kila mahali;
  Tatizo la umeme halieleweki, labda kila mwananchi atafute ufumbuzi wake.

  Nilivyomwelewa Waziri Mkuu ni kuwa mafungu ya "Other charges" kwenye wizara zote yatapunguzwa ili kupata fedha ya kutatua tatizo la umeme. Kwa maana nyingine mapato na matumizi hayatabadilika ili mgao hasa wa Other charges utabadilika kwa wizara zote.
   
 4. Bright Smart

  Bright Smart JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 644
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  aisee kweli hili swali pia na mimi nimevutiwa nalo kwa wenye ufahamu watujuze, very critical!!
   
 5. K

  Kifuna JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 426
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkulo hasomi bajeti nyingine kinachofanyika ni kuhamisha mafungu ya pesa kutoka kwenye bajeti ileile ya Madini na nishati ili mafungu hayo yatumike kwenye umememe. Mfano pesa zilizotengwa kwa ajili ya Poasho,Usafiri,Magali,Utafiti, Masurufu,Mafuta zote hizo zitahamishiwa kwenye umeme. Kwa kawaida Serikali huwa haifuti kodi hata kidogo inachokifanya ni kuihamisha kodi.Mfano wakipunguza kwenye Sigara ujue wameongeza kwenye Mafuta.
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Waziri Mkullo mwishoni kabisa ataleta marekebisho baada ya bajeti ya wizara zote kupita. Bajeti ya wizara ya maji nayo tunatarajia itakwama tu. Na Mwandosya mwenyewe bado yuko India.
   
 7. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama vifungu vitakuwa reallocated ni kwa ajili ya kununua mitambo ya dharura au kukodi?
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Fanya hesabu rahisi; Kama ilikwisha pitishwa na inatokana na kupitishwa kwa bajeti za wizara zote, je bajeti za wiraza zote zikipitishwa na marekebisho yake ina maanisha nini?

  I mean kama ulikubali kumempereka mwanao shule alipofika mwaka wa pili karo ikapanda kulinganisha na pale na ulipofanya maamuzi ya kumsomesha unafanya nini? unamwondoa shule au unaendelea kumsomesha hadi amalize masomo yake? Bajet kuu ni indications kama ingelikuwa sivyo kusingi kuwepo na bajeti za kila wizara, hivyo kupishwa kwake ndio kusema walipitisha development indicators and policies na wanapokuja kujadili bajeti za wizara wabunge wanaenda mbali zaidi kuangalia uhalisia na matarajio ya bajeti mama, what are strategies behind the indicators, wizara ina mipango gani, mbinu gani, mikakati gani etc etc, naona wewe unawaza fedha tu? bajeti siyo fedha peke yake fedha ni kiashiria tu? siyo halisi hata kidogo.
   
 9. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi ule Muswada wa Fedha (The Finance Bill) ulishapitishwa au utapitishwa baada ya Mkulo kufanya marekebisho ya Bajeti yake?
   
 10. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Mwandosya yupo India! Mbona walikuwa watowa taarifa humu kuwa ndie aliyekuwa ananunuwa madiwani wa CDM Mbeya last two days?
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ule ulishapita. Pengine JK kwa sababu ya kuzurula kwake hajapata muda akausaini. Ndege ya Mkapa inamzingua ile mbaya.
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Yuko India. Mgonjwa. Tatizo la maji Dar litampa taabu kwelikweli. Mh Mnyika hatamwachia kirahisi.
   
 13. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama alivyosema Mnyika jana nje ya ukumbi wa Bunge. Inabidi CDM wakomae irudishwe ili ijadiliwe upya, pia ile ya Mpango wa miaka mitano nayenyewe itakuwa imevurugika. Kazi kwelikweli.
   
 14. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mi ninavyojua bajeti mama ya Mkulo ikipingwa isipitishwe, Rais anavunja baraza la Mawaziri, sasa kwa hili sijui atampa lidanda Ngeleja au sijui itakuwaje...ngoja kwansa!!
   
 15. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ndugu think b4 inked...marekebisho machache ya wizara mbalimbali yanafanyika na yanaingizwa kwenye bajeti mama, na ndio maana baada ya bajeti husika kusomwa, inajadiliwa for some days then inapitishwa. Sasa hii ya Ngeleja ni tofauti, Bunge haijaipitisha kabisa..Imepingwa!! thtz the point
   
 16. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Ilishasainiwa na Mh. Raisi, spika aliwatangazia wabunge
   
Loading...