naomba mnitafutie kazi jamani

Ni vyema ukaweza kuwaambia watu hata kitu ulichosomea maana kusoma sua peke yake hakutoshi pale kuna kozi nyingi sana VET,HOMEC,FST,AGRIC,AGRIBUNINESS,ANIMAL SC. etc sasa wewe weka wazi tu hapa unaweza kukuta kuna mwajiri anataka watu wa aina yako ila kwa kuwa hujafafanua sana basi inakuwa ngumu sana kuweza kujua ni kitu gani unataka./
Thanks
 
watu mnaowapaga ushauri kama huo watu wanaotafuta kazi huwa mnanichosha!!!
Sasa mtu kazi hana, mtaji akatoe wapi jamani!?? Muelekeze japo namna ya kupata huo mtaji.

Mkuu. akutukane hakuchagulii tusi!!! Hapa huwa naikumbuka nyimbo ya Suma G inayoitwa Vituko Uswahilini!! Kuna sehemu anasema
"Msituletee hizo watoto wa kota watawadandia shingo, mnaona huku uswahilini mnauliza kuhusu Isidingo, mnataka tuwajibu naona mnakutuletea maringo"!

Wangejuwa jinsi watu tunavyo-strugle kwa kila posibility lakini tunajikuta tupo palepale wala wasingesema hayo mambo!! Nakumbuka 2009 lilitoka tangazao la Business Plan Competition!! Watu tukatumia hadi senti yetu ya mwisho kuandika Biz Plan, matokeo yanatoka hata kwenye 600 bora hatupo!!!! Kuna mshikaji ninamfahamu ambae kwao ni mambo safi, yeye akashiriki na akaingia kwenye hatua ya awali na akapewa pesa hiyo ya serikali!! For what i know hakuanzisha biashara yoyote na hela yote kala!!! Ana wasiwasu gani wakati ana kazi mzuri tu?! Watu ambao tupo serious hatukapata hiyo opportunity na katu sitaki kabisa kuamini kwamba Plan yangu ilikuwa mbaya! Naamini sikuwa na bahati lakini sio kwamba plan yangu ilikuwa mbaya! Na kama kuna mtu anaweza kui-finance plan yangu (ili mradi tusitiane changa la macho) with interest mie nipo tayari hata sasa!!! Hivi ni nani asiyejua source ya capital jamani? Hivi ni nani asiyejuwa kwamba familia zingine hata ugali wa kila siku ni issue kuupata?! Kwangu kuajiriwa haijawahi kuwa best option kabisa lakini nahisi sitakuwa na namna! Nakumbuka wakati nipo chuo nilisoma kwamba capital sources ni friends, ndugu, jamaa, wazazi na ikishindikana kabisa ndipo nenda kakope benki!!!Wengine opportunity hizo zote hatunazo, na for what i know hakuna benki nchi hii inayo-finance start up business; kama ipo na ambayo vile vile wanajali sana idea kuliko dhamana (kozi wengine hatuna dhamana wala kinachofanana na hicho) basi tuambiane wakuu coz' tumeshachoka kujidhalilisha kila siku kwenye maofisi ya watu ambao nahisi huwa wanafurahia zaidi wanavyoona tunawanyenyekea kuliko kuataka kutusaidia!!
 
duh! pole SUA coz gani mbona jamaa wengi wa sua atleast wana sehemu za kujishikiza? ingawa sio wote au mzee we unachagua? tafuta sehemu ya kujishiza mpaka mwezi wa saba wizara ya kilimo ina mpango wa kuajili watu kibao. hii wizara ina kazi nyingi we fanya kupeleka CV yako pale watakupa maelekezo ya kukusaidia. Vile vile keep in touch with ur friends wale uliosoma nao na wale waliokutangulia, kuna mtu anaweza kuitiwa kazi asiipende akakupigia pande wewe. mwisho hakikisha ulimi wako uachezacheza sana unapokutana na watu hasa usiowajua.
 
Pana Kampuni Makumbusho sio mbali kutoka kwenye GETI la kampuni inauza Matrekta.
Jina la hiyo kampuni X-S Marketing.Ingia pale jiunge nao.Usikate tamaa - utakachojifunza kitakusaidia kwa kipindi kirefu maishani mwako.

UTAKUWA NA "Confidence" big time

Usiache kuendelea kuomba kazi.
Mbeleni soma mambo ya Robert Kiyosaki 'Poor dad Rich dad dot com"
 
Mkuu nimesoma homec nimefanya field kiwakuki ambapo nilikuwa nashulikia na home based care activity pia nimefanya field cords centre for research and sustanable development, for now am volunteer at kilimanjaro volunteer which is an ngo
 
It could have been much better kama ungeandika unaomba msaada wa mbinu za kupata kazi; they are plenty!! kwa kukusaidia;
1. andaa CV yako vizuri (not more than 3 pages)
2. sambaza cv zako kwenye organisations that u think u are capable to work with e.g. kama una GPA >3.5 lete vyuoni
3. ukifocus sehemu, waweza enda kumuona manager physically then ndo ukamwachia na barua
4. hakikisha una excel when it comes umeitwa kwenye interview ( read tips/interview tactics)
nk.
 
pole sana ndugu yangu, haya ndiyo maisha ipo siku utatoka,hizi pesa hutuwezesha tu kuishi hapa duniani lakini we will all go with nothing to where we belong, sasa hebu cheki...... hii fungua google alafu tafuta kazi ikufaayo mitandao hii.
devenetjobs.
zoomtanzania
jamiiforum
naomba kazi
naukri.com

asante, wish u all the best kujenga taifa hili ukipata kazi uwe patriotic kwa nchi yako.tamaa mbaya.
 
Ulivyo andika inaonyesha umekata tamaa kwa kiasi kikubwa sana,NEVER GIVE UP!! Utapata tu chakarika na urushe details za course yako wa jf tutakusaidia.ELIMU HAIMTUPI MTU,BIDII YAKO TU NDIO INAHITAJIKA. :A S 2152:God bless you comrade!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom