Naomba mnisaidie. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba mnisaidie.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by The third, Dec 15, 2011.

 1. T

  The third Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mtu ka ukumiwa miaka kumi na tano jela kwa kosa la mauwaji baada ya kutoka jelakamu ona mtu yule yule aliye ukumiwa yeye kuwa kamuua ika bidi achukue pangaamufukuze uyo mtu alipo mkamata aka mkata mapanga mpaka akamuua, je?ata ukumiwa tena kwa kosa la mauaji?
   
 2. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  hebeu panga vizuri maandishi yako. ukiandika yasome kama yanaeleweka ndo u post, tukusaidie. maana nimeshindwa kuelewa, huyu aliyeuawa anauawa kwa mara ya pili au ?
   
 3. m

  moshingi JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwa jinsi ulivyoandika uzi wako ni vigumu kueleweka.
  Hatahivyo kama nitakuwa nimejitahidi kukuelwa, ni kwamba
  jamaa alifungwa miaka 15 jela kwa kosa la mauaji, alipotoka
  alikutana na yule mtu mbaye alituhumiwa kuwa alimuua yaani
  yule aliyepaswa kuwa "Marehemu" alikuwa bado yu hai na kwamba
  huyo jamaa aliyetokea jela akaamua kumkimbiza na kumkatakata
  kwa panga ili amuue akifikiri kuwa adhabu ya kumuua mtu huyo tayari
  alishaitumikia hivyo huenda hawezi kuadhibiwa tena.
  Kama "senario" ndiyo hiyo jibu lako ni kama ifuatavyo:

  Hapa Tanzania kosa la mauaji haliadhibiwi kwa kifungo cha miaka 15, adhabu
  ya chini ni kifungo cha Maisha. Vinginevyo huyo jamaa atakuwa alifungwa
  kwa kosa la Mauaji ya bila kukusudia " Manslaughter".

  Hata kama ni kweli yalifanyika makosa wakati wa upelelezi na ushahidi
  mahakamani ukatolewa kuwa "marehemu" alikufa kutokana na kitendo fulani cha
  mtuhumiwa, halafu imebainika baadaye kuwa hakufa mtu kwa kitendo hicho, haihalalishi
  kumuua sasa baada ya kumaliza kifungo na kumuona"marehemu" yupo hai. Hapo sasa atakuwa
  ametenda kosa kubwa la mauaji, kwani vigezo vitakuwa vimekamilika yaani, tendo baya + nia ovu.
   
Loading...