Naomba mnielewe tu

Naomba mnielewe tu

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,745
Reaction score
25,677
Nielewe tu
Binti mmoja aliwaambia wazazi wake kuwa ana mchumba na anakuja kujitambulisha, wazazi waliitana na kuandaa kila kitu lakini yule mchumba hakutokea, alitafuta udhuru wa ajabu ajabua na binti kwa aibu aliwaambia wazazi wake kuwa kapata matatizo atakuja wakati mwingine. Muda ulipita na binti aliendelea na mahusiano na yule Kaka ahadi zikiwa zilezile nakupenda, nitakuja, subiri hiki subiri kile.

Siku moja Bibi yake alimuita na kumuambia ni mwaka sas atangu utuambie una mchumba je bado uko naye au ushamuacha, binti akasema yuko naye lakini haoni kama kuna ndoa tena, anahisi mwanaume anampotezea muda. Bibi akamuuliza kama unahisi anakupotezea muda kwanini usimuache atakuumiza. Binti akamjibu “Bibi hawezi kuniumiza tena nishamjua hata akiniacha siumii tena hata mimi nampotezea muda tu sijali tena!” Bibi alitabasamu, siku iliyofuata Bibi alimuomba mjukuu wake kumsindikiza sehemu, waliondoka mpaka kufika sehemu kulikua na ndoo yenye maji mahcafu, Bibi akamuambia mjukuu wake kubeba binti alishangaa lakini bibi alimlazimisha akabeba, uchafu ulimdondokea na maji yalikua yakinuka sana, walitembea mpaka sehemu nyingine, wakakuta kuna ndoo ya maji masafi, Bibi akamuambia kuwa amsaidie kubeba tena, binti akamuambia hataweza kwani ana ndoo nyingine kichwani.

Bibi akamuambia kama hawezi basi waondoke na ile ya maji machafu, binti akasema waweke chini ile ya maji machafu ili wachukue masafi lakini Bibi alikataa alimlazimisha abebe zote, ile ya maji masafi akashika mkononi na ile ya machafu akaweka kichwani. Walitembea sana akachoka na kuachia ile ya maji masafi akabaki na machafu. Walifika nyumbani kachafuka na ananuka, Binti hakuelewa maana yake lakini Bibi alimuuliza kama kajifunza kitu akasema hapana!

Bibi alimuambia mjukuu wangu unapokua na mwanaume ambaye haeleweki ukaendelea naye na kudhani unampotezea muda tu ni sawa na kubeba ndoo ya maji machafu, unajua ni machafu lakini unabeba tu, ila kumbuka una kichwa kimoja, ukiwa na umebeba maji machafu unajizuia hata kubeba maji masafi na hata ukiyabeba kwa mkono basi utachoka tu na kuyaachia. Kama mwanaume unaona ni mzigo kwako unapoendelea kuwa naye unazuia nafasi ya mwanaume mwema kuja kwako
❤️
 
Hata sielewi elewi, hizi hangover sio poa!
Asubuhi njema jmn
 
Hangover sio poa..Nitasoma kesho[emoji4]
 
Dah...uzuri wa mwanaume anaweza kubeba ndoo 8 za maji machafu...na akiikuta ya maji safi anabeba tu...na haachi ndoo yoyote anayoikuta njiani[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kweli kabisa.
Bibi ametumia akili kubwa ila binti kwakuwa ni kichwa maji hakulijua hilo.

Ndivyo ilivyo kwa wadada wengi, wanaharibikiwa bila kujua. Siku wakijua muda unakuwa umeshawaacha mbali.
 
Back
Top Bottom