Naomba mchanganuo wa gharama za ujenzi wa nyumba ya chumba kimoja

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,022
4,220
Habari za wakati huu ndugu zangu.

Naombeni kujua MCHANGANUO WA GHARAMA za ujenzi wa nyumba ya chumba kimoja master na sebule kiwanja tayari Ninacho tofali Ninazotarajia kitumia Ni za cement (mchanga mtupu+cement)

Natanguliza shukrani zangu.
 
Habari za wakati huu ndugu zangu .

Naombeni kujua MCHANGANUO WA GARAMA za ujenzi wa nyumba ya chumba kimoja master na sebule kiwanja teyari Ni nacho tofali Ni nazo tarajia kitumia Ni za cement (mchanga mtupu+cement)

Natanguliza shukrani zenu
Kujenga wapi ?

Gharama zinatotautiana kulingana na location.
 
Msingi laki tatu boma 250,000 lenta 150,000 au kwa kila tofali TZS 500+ 200,000 ya usimamizi

Mkuu hii inakuwa ni chumba, sebule, jiko na Choo ndani au inakuaje kiongozi...?

Unaweza kuwa na picha ya mfano wa nyumba itakavyokuwa/itakapomalizika mkuu...?

Natanguliza shukran.
 
Chumba sebule,Jiko na Choo,Ukubwa wa Chumba ni futi 10.Sina Picha yake.Ila kama una pesa iko ambayo unaweza kumalizi na kuhamia kwa gharama ya Milioni 9.5.Tuwasiliane PM kama utapenda.Imeshaezekwa na Madirisha,Iko Gezaulole Kigamboni
 
Sawa kiongozi ila kama nina eneo ambalo nitajenga kuanzia mwanzo si inaweza gharama yake kuwa chini ya hapo boss...?
 
Kwa hili eneo na jinsi nyumba ilivyo haiwezi kuwa chini ya hapo.Huyu anauzia shida ndo maana.Hizo hesabu nilizokupa zisikufanye ukaona ni nafuu ujenzi una constraints nyingi sana
 
Chumba sebule,Jiko na Choo,Ukubwa wa Chumba ni futi 10.Sina Picha yake.Ila kama una pesa iko ambayo unaweza kumalizi na kuhamia kwa gharama ya Milioni 9.5.Tuwasiliane PM kama utapenda.Imeshaezekwa na Madirisha,Iko Gezaulole Kigamboni
Tofali 800,Cement mifuko 30 Bati 25,Nondo pcs 11,Maji,Misumari,Mbao Futi 250(2by3) na futi 100(2by2

Unataka nini kingine?
Mifuko 30 kwa matofauri 800?, Anajenga jengo la serikali?, Hapa inaonesha mfuko mmoja utajenga tofari 26,uswahilini tunajenga tofari 50 mpaka 55 kwa mfuko moja wa cement
 
Wewe unazungumzia uswahilini,Pili unatakiwa ujue kwamba hii ni estimates ambayo inhusisha,msingi,mkanda wa chini,lenta so think again kabla hujaleta ya uswahilini.
 
Tofali 800,Cement mifuko 30 Bati 25,Nondo pcs 11,Maji,Misumari,Mbao Futi 250(2by3) na futi 100(2by2

Unataka nini kingine?
ndugu umekadiriaje hapo wakati hata vipimo hajatoayawezekana hizo tofali zikawa za msingi tu zikabaki kidogo.
nondo hapo pia utata
 
Back
Top Bottom