Naomba mawazo yako kwenye hili

Malovee

JF-Expert Member
Dec 3, 2020
202
324
Habari, hii ni habari ya kweli kabisaa, niliunganishwa na best friend wangu katika kazi Fulani, nilifurahi Sana kutokana na wakati huo nilikuwa na uhitaji wa kazi.

Rafiki yangu hiyo naweza sema.ni mtummwenye moyo wa kipekee Sana maana,kibongobongo ni ngumu rafiki kukupeleka sehemu yenye ulaji aliyopo yeye pia.

To cut the story short, tulifanya kazi pamoja Kwa muda Kama wa miezi sita katika kampuni hiyohiyo, baadae ikatokea wanapunguza wafanyakazi na rafiki yangu akawemo katika kundi Hilo na Mimi nikabaki.

Niliumia Sana kutokana na hilo, but niliahidi kuwa pamoja Naye katika shida na raha kwa kadri ya uwezo wangu.nikitoa kiasi Cha pesa Kila mwisho wa mweZi kupatia yeye Kama shukurani tu.

Ikatoakea mweZi mmoja sikumpatia kiasi Cha pesa Kama ilivyokawaida kutokana na mm kubanwa ,kulipa Kodi,kusomesha mdogo wangu na vingine vingi,nikamweleza jinsi ilivyo.

Baada ya kumuelez ahivyo, alikasirika sana na kuniporomoshea matusi, ikiwepo na kwamba nimejiona nimefika, na bila yy nisingejuwa hiyo kampuni.nilimsihi Sana na kumwambia kwamba natambua msaada wake.

Wakuu imefikia hatua mpaka natamani kuacha hiyo kazi kwajinsi anavyonisimanga Kwa ndugu jamaa na marafiki.mpaka tunaandiak hapa mm na rafiki yangu hiyo ni Kama paka na panya, amenijengea chuki ya ajabu nashindwa nifanyeje.

Naomba mawazo yenu nifante nini ,maana najiona kama.mtumwa kupitia kazi hii.
 
Tuliza munkari usipaniki endelea na majukumu yako kama kawaida.

Kama kuomba kazi utaomba kwa muda wako ikitokea ila sio kwa influence ya mtu mwingine.

Na pia wala usimlaumu huyo jamaa kuwa mkali hivyo,hiyo changamoto anayopitia ni ngumu sana ndio maana unaona anabadilika na kuwa mbogo.

Kusimamishwa kazi ghafla kwa wakati usiotegemea na huna njia mbadala huwa ni janga zito sana lazima avurugwe.

Cha msingi ukiwa na uwezo wa kumsaidia msaidie ila ikishindikana basi usilazimishe ukajikandamiza pia utakosa amani.
 
Mnakaa karibu kiasi cha kuwa mnaonana mara kwa mara mpaka uwe na sononeko hivyo?

Hey tell her/him you've alot of bills to pay, mambo yamekuwa tight sana umebanwa.

Asipokuelewa piga block ndio nini sasa kuwa mtumwa wa msaada wake? Ni sawa alikusaidia ila juhudi zako pia zimeplay part yake huko ofisini ndio maana ukabakizwa.

Aache uswahili.
 
Mnakaa karibu kiasi cha kuwa mnaonana mara kwa mara mpaka uwe na sononeko hivyo?

Hey tell her/him you've alot of bills to pay, mambo yamekuwa tight sana umebanwa... Asipokuelewa piga block ndio nini sasa kuwa mtumwa wa msaada wake? Ni sawa alikusaidia ila juhudi zako pia zimeplay part yake huko ofisini ndio maana ukabakizwa.

Aache uswahili.
Nimemueleza na chuki ndiyo imeanzia hapo
 
Ni ushauri mzuri

Hali ngumu na anaitaji kuombewa Ni stress anataka kuzitolea kwa jamaa

Ila anashindwa kujua ridhiki anatoa Mungu unapo msaidia MTU usitegemee kulipwa Mungu atakubariki kwa namna yke
Muombee kwa Mungu anapitia wakati mgumu sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom