makinikia 101
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 491
- 876
Wakuu mbalimbali naomba nianze kw kuwek baadhi ya vifungu kama ilivyo kwwnye CPA:Mkuu nimepata la kuchukua hapa, asante. Sasa tusaidie tena, ni kweli walio mtaani ushaidi unakuwa bado?
Na je ni kweli wanaosemwa ushaidi umekamilika wakienda mahakamani ushaidi huwa bado ama nini huwa kinasemwa bado upelelezi unaendelea?
Na ni kweli kinachotekea mahakamani ni pesa zaidi ya kuliko haki? Make hata wewe naona unakazia sana maamuzi ya mahakama kudhoofishwa kati ya wenye nazo dhidi ya waso nazo, unamaanisha hukumu nyingi ni matokeo ya pesa na si matakwa ya kisheria ilivyo?
Na swali la mwisho kwa leo
5. Naelewa kuna kesi zinatakiwa kuanzia mahakama za wilaya n.k lakini pia kuna kesi zinapelekwa mfano kisutu wakati hii mahakama haina nguvu ya kusikiliza na kutoa hukumu juu ya baadhi ya kesi. Ni
kwanini hizo kesi huwa hazipelekwi moja kwa moja kwenye mahakama stahiki badala ya kuanza kuzungushana kuanzia kwingine alafu ndo baadae muhamishiwe kwingine?
Nishukuru na niishie hapa ila nitarudi siku nyingine kwa ajiri ya kutafuta uelewa zaidi kutoka kwenu wanasheria.
"171.-(1) Pale ambapo chini ya masharti ya Sheria hii
mahakama ya chini inayoongozwa na Hakimu wa Wilaya itamtia
hatiani mtu mzima yeyote kwa kosa iwapo, baada ya kupata taarifa
kuhusiana na tabia yake na mengineyo kuhusu mtu huyo mzima au
kuhusiana na mazingira ya kosa, mahakama ina maoni kuwa adhabu
kubwa inatakiwa kutolewa kwa kosa zaidi ya ile ambayo mahakama
ina mamlaka ya kutoa, mahakama inaweza, badala ya kumshughulikia
kwa namna nyingine yoyote, kumweka mhalifu chini ya ulinzi wa
Mahakama Kuu kwa adhabu
kufuatana na masharti yafuatayo ya
kifungu hiki.
(2) Pale ambapo mhalifu anapelekwa Mahakama Kuu kwa
adhabu chini ya masharti ya kifungu hiki,Mahakama Kuu itachunguza
mazingira ya kesi na itamshughulikia mhalifu kwa namna ambayo
mtuhumiwa huyo angeshughulikiwa na Mahakama Kuu iwapo
angetiwa hatiani na Mahakama Kuu kwa kosa hilo."
Lakini ikumbukww kwamba kesi itakua inatajwa tu kutakua hakuna usikilizaji wa shauri katika mahakama ya chini.
Vilevile sijaweka bandiko lolote lenye kuhusianisha sheria na pesa, lahasha mkuu. Nimesema wakili mzuri anawwza kukusaidia kwwnye kesi ngumu. Zingatia kina mzee wa vijisenti, zingatia Lulu and the list continues. Sisi maskini muda mwingne kwa maana ya uchumi tukashindwa kuwapata mawakili wa kutunasua (mana wana gharama kubwa pia) ndo mana tunaanguka.
Nikushukuru mkuu