Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 1,448
- 1,003
===
Bunge limepitisha Mabadiliko muhimu ya Sheria kupitia muswada wa mabadiliko ya Sheria mbalimbali Na. 7 wa mwaka 2021 ambapo kifungu cha 131 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kimefanyiwa mabadiliko.
Kifungu hiki kipya cha 131A kinamkataza Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP), Polisi, au yeyote mwenye mamlaka ya kushitaki, kutokupeleka kesi mahakamani pasipo upelelezi kukamilika. Hii ilipelekea mtu kukaa na kesi kwa miaka mingi huku kila siku akiambiwa na waendesha mashitaka kuwa upelelezi haujakamilika.
Pia kwenye mabadiliko haya, ikiwa utashitakiwa na mahakama kukuachia huru, basi polisi hana mamlaka ya kukukamata tena na kukufungulia kesi upya. Kitendo hiki kilikuwa kinawafanya watu watoke mbio sana mahakamani mara baada tu ya kuachiwa huru.
Kwa msingi huu Mwendesha mashtaka wa serikali, Polisi, na wengine wote wenye mamlaka ya kushitaki, ikiwa hajakamilisha upelelezi hana haki ya kufungua kesi mahakamani hadi pale atakapokamilisha upepelezi na pia hawezi kukukamata ikiwa umepatikana huna hatia na mahakama.
Unaweza ukaniuliza ikiwa wamekatazwa kupeleka kesi mahakamani kabla upelelezi haujakamilika, ina maana sasa watuhumiwa watasota sana selo mpaka polisi wakamilishe upepelezi wa makosa yao?
Jibu ni hapana, mabadiliko hayo hayo kifungu cha 131A (2) kinasema kuwa ikiwa upelelezi haujakamilika na hivyo kutomwezesha mtu kupelekwa mahakamani basi anatakiwa aachiwe kwa kupewa dhamana wakati polisi ama mamlaka nyingine ikiendelea kukamilisha upelelezi wa makosa yake. Hautakiwi kuwekwa selo au kukaa polisi ikiwa upepelezi wa kosa lako haujakamilika.
Hata hivyo, katazo hili la kutopeleka kesi mahakamani bila upelelezi kukamilika linahusu makosa yote isipokuwa makosa ya kubaka (rape), wizi wa kutumia silaha (armed robnery), kumiliki silaha kinyume cha sheria, kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria, makosa ya kujeruhi sana (grievious harm), kosa la kuhatarisha usalama wa taifa, usafirishaji dawa za kulevya, na jinai nyingine ambazo hadhi yake husikilizwa tu na mahakama kuu. Kama kesi yako imefunguliwa mahakama kuu basi kosa hilo haliguswi na mabadiliko haya, utaratibu wa kawaida wa mashauri ya jinai utafuatwa.
Kifungu cha 131A(3) cha mabadiliko haya kinatoa msisitizo kwenye kifungu cha 170(6) cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kwamba kama makosa ambayo adhabu zake kama mtu angekuwa anahukumiwa na mahakama angehukumiwa kulipa faini ya Tshs 200,000/= basi mtu huyo anatakiwa akiri kosa kwa maandishi, kisha alipe faini hiyo kwenye akaunti za serikali, na aachiwe huru.