Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 16,958
- 7,512
Leo mimeona niweke haya mambo kwenu ili nipate kuelewa vyema, wanasheria naomba mnisaidie
1. Ni kwanini mtu anapelekwa mahakamani kabla ushaidi haujakamilika?. Tumeona kesi nyingi sana zikizungushwa kwa mda mrefu sana eti kisa ushaidi haujakamilika, kama ushaidi haujakamilika ni kwanini ashitakiwe na kuanza kuzungushwa mahakamani wakati bado mnaomushtaki hamna ushaidi wa kutosha?
2. Naangalia kesi ya Kenyatta na Ruto kule ICC, mbona hawa walikuwa wakihudhuria kesi kutokea makwao kisha wanarudi walikotoka. Kwanini huu utaratibu usitumike hadi pale huyo mtu atakapobainika kuwa na hatia ndo ahamishiwe sero?
3. Ninaangalia kesi za akina EPA, IPTL na ESCROW. Mara nyingi wananchi tumehoji ni kwanini wahusika hawapelekwi mahakamani na kila wakati yamekuwepo majibu yasiyo ridhisha kabisa. Mara nyingi TAKUKURU wamekuwa wakisema hawawezi kuwapeleka mahakamani hadi pale ushaidi na upelelezi utakapokamilika. Swali, kama hivyo ndivyo ni kwanini mfano leo tunaona akina Seth na Ruge wamepelekwa mahakamani na kila siku wanapigwa tarehe tukiambiwa bado upelelezi haujakamilika. Iweje hawa wamepelekwa japo upelelezi haujakamilika na watuhumiwa wengine wameachwa mtaani kwa kisingizio kile kile? Ni nini sasa maana ya upelelezi kukamilika ili mtu apelekwe mahakamani na upelelezi kutokukamilika mtu anaendelea kusoteshwa rumande?
4. Mtu anayepelekwa sero wakati kesi ikiendelea na baadae ikaonekana hakuwa na hatia na akaachiwa huru huku ameishi sero mda mwingi tu, huyu mtu huwa anastahili kulipwa na huwa analipwaje na sana sana pale anapokuwa alishtakiwa na serikali?
Kwa leo nakomea hapa kwanza ....