Naomba maana ya maneno haya

Mu-Israeli

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
2,454
975
Wana JF,
Nimekuwa niliyasikia maneno haya mara kwa mara yakitumika.
naomba maana yake.
Maneno yenyewe ni kama ifuatavyo:-
  • Zingua
  • Mzuka
  • Swaga
  • Gozi-gozi

Asenteni sana wana JF.
 
Wana JF,
Nimekuwa niliyasikia maneno haya mara kwa mara yakitumika.
naomba maana yake.
Maneno yenyewe ni kama ifuatavyo:-
  • Zingua
  • Mzuka
  • Swaga
  • Gozi-gozi

Asenteni sana wana JF.
.
Mu-Israeli

Haya tena haya ni mambo ya Kiswahili cha mtaani.

Mimi ntakusaidia kukuongezea maneno yanayoendana na hayo ili kwamba kupitia hayo utaweza kujua maana ya maneno hayo pamoja na kukuongezea maneno memngine ya mtaani yenye maana sawa.

1. Zingua inaendana na mapepe, mchecheto, wenge, data, pagaisha, datisha

2. Mzuka inaendana na mkinga, tumbo joto, noma, soo, ndita, panda kichizi, chimba biti;

3. Gozigozi = kiwingu

Inamaanisha bania, punja mtu kitu ambacho anastahili kupewa, nyima mtu kitu (reduce the share somebody), Unanibania. Unanipunja, hutaki niendelee.

Hali ya kumzibia riziki mtu,poteza muda, zubaa.

Mfano:

1. Ameniletea gozigozi. = Amenizibia riziki yangu.
2. Usiniwekee gozigozi. = Usinizibie riziki.
3. Acha gozigozi. = Acha kuzubaa.​

= kiwingu, bania​


4. Barida = baridi, shwari cool


Derivation from SS *baridi 'cool, cold', by change of final vowel -i to -a. Not common

Mfano:
Hali vipi? - Barida tu mwana. Hali vipi? - Poa tu rafiki.

> baridi, poa, shwari

5. Beki tatu = msichana wa kazi, mfanyakazi wa ndani housegirl

Metaphorical or metonymic extension of football player on position "back 3" (sweeper).

Mfano: Beki tatu wa kina Juma ni magoli! = Msichana wa kazi wa kina Juma ni mzuri sana!



6. Chenza = mwanamke asiye bikira = woman who is not a virgin

Metaphorical extension of *chenza 'tangerine'' Used in contrast to *chungwa (orange) denoting a virgin. Concept: A tangerine is easier to peel than an orange.


Mfano: Hoya lile ni chenza. = Hoya, yule ni mwanamke asiye bikira.

7. Chungwa = mwanamke bikira = virgin

8. Golikipa:


1. Mama wa nyumbani (housewife)​
2. Mtu ambaye anapokea tu, mtu ambaye anasubiri vitu vya kuletewa (someone who is only receiving)​

Metaphorical extension of 'goalkeeper'.


1. Unajidai hutaki kuwa golikipa.
2. Golikipa ni mgonjwa (Mke wangu, mama wa nyumbani, ni mgonjwa)
3. Nisalimie golikipa. (Nisalimie mke wako, mama wa nyumbani).​
 
Back
Top Bottom