Aen Urner
JF-Expert Member
- Aug 31, 2016
- 388
- 380
Naandelea na masomo yangu ya chuo kikuu Udsm nikiwa mwaka wa kwanza namshukuru mungu ni mmoja ya wanafunzi wanaofadhiliwa na Loarn Board katika masomo lakini kitu kinachonifanya nisijisikie vizuri ni kuona wanafunzi wenzangu wanavyopata tabu na kuhangaika juu ya mkopo kuna wengine walilipoti chuo kabisa bila kujua hatima yao mpaka batch zote zimekwisha na wamehamua kuappeal na hawajui hatima yao bado wanapitia ugumu sana hapa chuoni kwani wamekaa muda mrefu sana bila kusajiliwa na kadri muda unavyokwenda ndivyo mambo yanakuwa magumu sana,
Tayari nimeshuhudia baadhi wakifungasha vilago kwenda kusikojulikana...kusikojulikana kwa sababu wengi wao husema hawawezi kurudi tena nyumbani kwao, Lakini kitu kingine ni laana hii inayotolewa na hawa vijana sio hao waliokosa mkopo tu mpaka wenye mkopo nao wanatoa laana zao kwa dereva wa lorry ni kawaida sana kupita mahali ukasikia maneno haya "Ngoja tu 2020 kitaeleweka" sijui hiyo 2020 kuna nini ila kama kuna mtu anafahamu niko tayari kufahamisha pia
Maneno hayo kwangu ni kama laana nitumie fursa hii kuiomba serikali kuliangalia swala hili kwa sababu ninaamini serikali nzuri ni ile inayosikiliza raia wake na mwisho wanaombea muujiza uwatokee wanafunzi wote katika vyuo vyote wanaotaka kusitisha masomo kwa sababu ya kukosa mkopo, tofauti na hapo wasubiri 2020 watapata tu.