Naomba kuuliza

kacnia

JF-Expert Member
Sep 16, 2014
4,024
15,784
wadau wa elimu nina maswali ambayo naomba msaada wenu kuyajibu na ikiwezekana kwa reference!

(1)ni mwezi wa ngapi mitihani ya kumaliza kitado cha sita 2017 itafanyika?

(2)je program ya kwenda jkt kwa wahitimu wa kidato cha sita bado ipo?

(3)je ni kweli kwamba muhitim yeyote wa kidato cha sita hataweza kujiunga chuo kikuu bila kuwa na division1&2 only? kama ndio hawa wengine watatakiwa kufanyaje kuendelea na masomo ya ngazi. za juu?

NATANGULIZA SHUKURANI NYINGI.
naomba kuwakilisha.
 
Mwenyewe sijui, natamani kujua, maana kuna Dogo hapa anakaa kaa tu kizembe sasa sijui anajiandaa kutaga coz hasomi! Ngoja wajuzi watujuze
 
1. Mitihani ya kidato cha sita ( school and private candidates_) inaanza trh 3/5/2016. Kwa uhakika tembelea web ya necta washaiweka ratiba unaweza kudownload na kuipitia kwa makini pia ucheck na grade mpya uzijue.
2. Hilo la jkt hadi sasa linazungumzwa kimazoea tu ila tamko halijatoka coz serikali iliyopo ni mpya so inaweza kuwepo kama kawaida, kurekebishwa au kutokuwepo kwa kuwa hilo suala ni la kisera zaidi. Hivyo basi jiandae kwa lolote.
3. Hizo ni tetesi ingawa kupata div 3 kunamfanya mtu awe limited ktk selection za vyuo kutokana na cutt points zinaxohitajika. Hivyo ni bora ukaze tu ili upate hayo madaraja ya juu la sivyo utakua unahangaika kwani ukitaka elimu mbadala ya degree zipo nyingi tu ukishahitaji watu watakushauri ila sio sasa kwa sababu utajiandaa kufeli.
Kwa uelewa wangu naishia hapo na yeyote anaweza fanya editing ya nilichozungumza.
 
Shukran sana mkuu kwa msaada wako lakini ninaombi kwako kama inawezekana
Naomba unipatie orodha ya vyuo vinavyochukua madaraja ya juu na vile vinavyochukua ya chini.

Natanguliza shukrani
 
Back
Top Bottom