mazongera
Member
- Jan 17, 2015
- 66
- 80
Ni shule wasichana mabwepande (Tumaini). Waalimu wamebuni chanzo cha kijiongezea kipato maisha yasonge.
Hii ni shule ya boarding kwa wasichana, kidato cha tano na sita. Mwaka huu baada ya shule kufunguliwa mwezi August, wale wanafunzi waliotoka kidato cha tano na kuingia kidato cha sita, walifanyiwa mitihani ya majaribio.
Matokeo ya majaribio hayo hayakuwa mazuri Sana,ndipo waalimu walipoona fursa ya kuwashirikisha wazazi kwa kuita kikao cha wazazi ili wazazi waone ni namna gani kwa kushirikiana na waalimu wapate ufumbuzi wake.
Baada ya waalimu kuiwasilisha hoja kwa wazazi,waalimu waliondoka na kuacha wazazi wajadili namna gani mzuri watakayoona inafaa ya kuwawezesha waalimu WAWAPAMBANIE WATOTO WAO.
Maazimio ya kikao, wazazi walikubaliana kila mzazi kuchangia 80,000/= elfu themanini ili kuwapa motisha waalimu wapate kutimiza majukumu Yao vizuri. Na hii ilipendekezwa itolewe kwa awamu mbili.
Nirudi kwenu wadau wa jamiiforums,
Je ni sahihi kweli kwa hiki walichokifanya hawa waalimu? Inakuwaje jukukumu linalohusiana na wao mzigo anakuja kubebeshwa mzazi? Utendaji kazi wa mwalimu kwa mwamafunzi wake unaonekana kwenye matokeo.
Upowapi uwajibikaji na uchapakazi wao waalimu hawa? Hivi wakaguzi wa hizi shule mpo? Mishahara wanayolipwa waalimu hawa inatokana na Kodi za hawa wazazi ambao leo wamegeuzwa ng'ombe wa maziwa. Hebu naomba waalimu timizeni wajibu wenu. Tupo kwenye maisha ya kupita tu kama unaona kipato hakitoshi tafuta kwengine tuwahurumie hawa wazazi wanapambana na mengi.