Naomba Kuuliza; Ni Udhaifu Wa CCM au Uimara Wa CHADEMA? Na tuunganishe dots! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba Kuuliza; Ni Udhaifu Wa CCM au Uimara Wa CHADEMA? Na tuunganishe dots!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMBOTA, Nov 3, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Nianze makala yangu kwa kuwapa pole watanzania wenzangu hasa kutokana na kupanda kwa gharama za maisha nasema POLENI WATANZANIA! .Kinachonifanya kushuka jamvini muda huu ni kujaribu kulileta kwwenu swala la mustakabali wa taifa letu hususani katika mwelekea wa kisiasa wa siku zijazo.

  Mwelekeo huu na hamu yangu ya kutaka kutambua ukweli na pengine kuunganisha dots ili kufikia tamati yenye mantiki imejikita zaidi katika vyama vya CHADEMA na CCM ambavyo kwa jinsi hali ilivyo ni dhahiri kuwa ndivyo vyenye nguvu zaidi kwa nyakati hizi.

  Nimekuwa nikijiuliza maswali fikirishi ikiwa hii hali ya kisiasa nchini kiini chake ni nini? je ni udhaifu wa CCM? , ikiwa nikikubaliana na hoja hii basi linaibuka swali lingine, iwapo ni udhaifu wa CCM mbona kwenye majimbo ya hayo makundi hasimu ya CCM kote wameshinda CCM? na je mbona 1995 NCCR ilikuwa tishio ingawaje hakukua na hiko kinachoitwa udhaifu au makundi? je tatizo lilikuwa nini?

  Na iwapo nikitaka kuamini kuwa ni uimara wa CHADEMA , baado nina maswali kadhaa, je 1995 NCCR ilipofanya vizuri what was the motive behind? je kwanini 2005 CHADEMA haikufanya vizuri? nini kiliongezeka 2010?. Naamini majibu ya maswali haya yatatufanyakama taifa kutambua mwelekeo wa siasa za nchi kwa siku zijazo na hivyo kuishi tukiwa na vision ya kimaendeleo kwa kuzingatia historia yetu na mwelekeo wetu kama Taifa.
  www.novakambota.com
   
Loading...