Naomba kuuliza: Baraza kuu la Chadema linaundwa na kina nani?

Changamoto2015

JF-Expert Member
Oct 1, 2012
773
313
Naomba kufahamishwa ili niweze kupiga hesabu zangu vizuri. Nasikia Zitto anampango wa kukata rufaa ili shauri la msingi lisikilizwe na baraza kuu la chadema. Je, kwa msingi upi anaamini haki itatendeka kupitia baraza hili lililopo ndani ya Chama alichokipeleka mahakamani?

Ni wazi kuwa baada ya Uamuzi wa leo wa Jaji John Utamwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania juu ya maombi ya Zitto Kabwe, Zitto anaelekea Baraza Kuu la chama hicho kwa ajili ya kusikiliza rufaa yake ya kuvuliwa nyadhifa zake chamani. Ni muhimu kujua, angalau, wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA.

Ibara ya 7.7.11 ya Katiba ya sasa ya CHADEMA inaainisha Wajumbe wa Baraza Kuu. Bila ya kuongeza au kupunguza maneno, naona ni vyema nikaiweka hapa kama ilivyo. Inasomeka:

7.7.11 Wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa watakuwa:
(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu.
(b) Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, Mikoa.
(c) Wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa kushauriana na Katibu mkuu na kuidhinishwa na baraza kuu. Wajumbe wateule hawa watateuliwa kwa uwiano wa wajumbe wanne wanaume wawili na wanawake wawili.
(d) Wajumbe watano watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la Chama, kwa uwiano wa wajumbe wanne toka Bara na mmoja toka Zanzibar kwa kila Baraza.
(e) Wenyeviti wa wilaya za chama
(f) Mwakilishi wa jimbo na chama

Kimsingi, hawa ndio watakaosikiliza na kuamua juu ya rufaa ya Zitto atakapoiwasilisha kwao. Mchakato wa kichama bado unaendelea.
 
naomba msaada,tofauti ya kamati kuu na baraza kuu la cdm,je wajumbe wa cc ndo hao hao wa baraza kuu,pia naomba kujua wajumbe wa baraza kuu wanapatikana vp?
 
Habari wadau,

Natoa ushauri kwa viongozi wa CHADEMA kuitisha kikao cha Baraza kuu haraka iwezekanavyo ili kuepuka kutoa muda ambao unaweza kutoa mwanya kwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama kuhujumiwa.

Msisahau wajumbe hawa ni kutoka sehemu mbali mbali nchini na wenye hali tofauti za kimaisha na mitizamo katika hii issue.

Wote mnajua watu walio nyuma ya Zitto na mienendo yao.

Any delay coud mean a disaster for the party.
 
Hahahaaa! Huu ndo Uchaguzi Mkuu wa Mwenyekiti wa Chadema!

Baraza likiamua Zitto arejeshewe Vyeo vyake Basi Slaa na Genge lake ndo mwisho wao.

Baraza likiridhia Zitto kuvuliwa vyeo vyake basi ndo Mwisho wa Zitto na Genge lake.
 
Naomba kufahamishwa ili niweze kupiga hesabu zangu vizuri. Nasikia Zitto anampango wa kukata rufaa ili awa jamaa wasikilize shauri lake la msingi. Je, kwa msingi upi anaamini haki itatendeka kupitia baraza hili lililopo bado ndani ya Chama alichokipeleka mahakamani?
baraza linaundwa na
w/viti wote wa mikoa

w/viti wa wilaya
 
kwa mujibu wa MEANDU: 7.7.11 Wajumbe wa Baraza
Kuu la Taifa watakuwa: (a) Wajumbe wote wa
Kamati Kuu.
(b) Wenyeviti wa Baraza la
Uongozi, Mikoa.
(c) Wajumbe wateule
wasiozidi sita watakaoteuliwa na
Mwenyekiti
wa Taifa kwa kushauriana
na Katibu mkuu na
kuidhinishwa na baraza kuu.
Wajumbe wateule hawa watateuliwa kwa uwiano
wa wajumbe wanne
wanaume wawili na
wanawake wawili.
(d) Wajumbe watano
watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila
Baraza la Chama, kwa
uwiano wa wajumbe wanne
toka Bara na mmoja toka
Zanzibar kwa kila Baraza.
(e) Wenyeviti wa wilaya za chama
(f) Mwakilishi wa jimbo na
chama
 
Last edited by a moderator:
Wadau kwan wajumbe wa kamati kuu na baraza kuu la chadema n tofauti
maana naamin uamuz utakuwa ule ule
watusaidie kututolea msalit zzk
 
Aaa nami naenda mahakamani ili niwpate kuwa mwanasiasa mahiri. Maana siasa bila sheria haiendi. Siasa ni test ya watu bwana sio umahiri wa sheria ama msabaha, matayo, mwinyi wangepinga kuvuliwa uwaziri.
 
Zzk anakawiza maziko yake tu, baraza kuu la chadema lilishaamua tangu 2010 kumvua uanachama mheshimiwa mbowe kamtetea, sijui sasa ni zamu ya dr slaa kumtetea au la
 
Wadau kwan wajumbe wa kamati kuu na baraza kuu la chadema n tofauti
maana naamin uamuz utakuwa ule ule
watusaidie kututolea msalit zzk

Hata kama uamuzi utakua ule ule lakini zitto atakuwa kawafundisho somo viongozi wangu, somo kwamba taasisi huongozwa kwa TARATIBU na sio kwa hisia, chuki na fitina.

tunawapa nguvu kina lukosi wanaosema chama chetu ni saccos, na inaumiza sana kuona taratibu hazifuatwi
 
Wadau kwan wajumbe wa kamati kuu na baraza kuu la chadema n tofauti
maana naamin uamuz utakuwa ule ule
watusaidie kututolea msalit zzk

7.7.11 Wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa watakuwa:

(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu.
(b) Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, Mikoa.
(c) Wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa kushauriana na Katibu mkuu na kuidhinishwa na baraza kuu. Wajumbe wateule hawa watateuliwa kwa uwiano wa wajumbe wanne wanaume wawili na wanawake wawili.
(d) Wajumbe watano watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la Chama, kwa uwiano wa wajumbe wanne toka Bara na mmoja toka Zanzibar kwa kila Baraza.
(e) Wenyeviti wa wilaya za chama
(f) Mwakilishi wa jimbo na chama
 
Wadau kwan wajumbe wa kamati kuu na baraza kuu la chadema n tofauti
maana naamin uamuz utakuwa ule ule
watusaidie kututolea msalit zzk

Baraza Kuu wajumbe ni:
1.Wenyeviti wa Mikoa
2.Wenyeviti wa Wilaya
3.Wakuu wa idara
4.Mwenyekiti wa Taifa
5.Makamu Mwenyekiti-Bara
6.Makamu Mwenyekiti-ZNZ
7.Katibu Mkuu

Technically Zitto kapoteza Ubunge wake maana BARAZA KUU litamfukuzia mbali ingawaje hela nyingiiii sana itapenyezwa kutoka CCM kwa hawa wajumbe!
 
Habari wadau,

Natoa ushauri kwa viongozi wa CHADEMA kuitisha kikao cha Baraza kuu haraka iwezekanavyo ili kuepuka kutoa muda ambao unaweza kutoa mwanya kwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama kuhujumiwa.

Msisahau wajumbe hawa ni kutoka sehemu mbali mbali nchini na wenye hali tofauti za kimaisha na mitizamo katika hii issue.

Wote mnajua watu walio nyuma ya Zitto na mienendo yao.

Any delay coud mean a disaster for the party.

Mods hii habari ina uhusiano gani na hii thread mpaka muiunganishe?!

Mods be fair

CC: Invisible
 
Last edited by a moderator:
Zito atashinda kwa uchawi sio kwa kuonga,jini mahaba zito
 
Nitashangaa sana kama baraza kuu kama watamsamehe zitto wakati kakipeleka chama mahakamani!
 
7.7.11 Wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa watakuwa:

(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu.
(b) Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, Mikoa.
(c) Wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa kushauriana na Katibu mkuu na kuidhinishwa na baraza kuu. Wajumbe wateule hawa watateuliwa kwa uwiano wa wajumbe wanne wanaume wawili na wanawake wawili.
(d) Wajumbe watano watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la Chama, kwa uwiano wa wajumbe wanne toka Bara na mmoja toka Zanzibar kwa kila Baraza.
(e) Wenyeviti wa wilaya za chama
(f) Mwakilishi wa jimbo na chama
Ndio maana Mbowe na vibaraka wake wakiangalia hiyo timu wanajua hawachomoki.
 
Back
Top Bottom