Naomba kusaidiwa ushauri juu ya maziwa

sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,283
976
Natanguliza heshimu.

Mara zote huwa naamini katika intelligency ya baadhi ya wana JF. Ushauri tunaopata hapa umetusaidia wengi kwa namna moja au nyingine.

Ndg zangu, leo naomba nishauriwe namna ya kutambua maziwa yaliyochakachuliwa, yaani yenye maji. Maana mengine sio rahisi kuyagundua. Kama kuna kifaa maalum au njia ya asili ya uhakika.

Pili, namna gani naweza kuhifadhi maziwa kwa muda mrefu yasigande pasipo kuyachemsha?

Shukurani zinatangulizwa wakuu!
 
Natanguliza heshimu,
Mara zote huwa naamini katika intelligency ya baadhi ya wana JF. Ushauri tunaopata hapa umetusaidia wengi kwa namna moja au nyingine.

Ndg zangu, leo naomba nishauriwe namna ya kutambua maziwa yaliyochakachuliwa, yaani yenye maji. Maana mengine sio rahisi kuyagundua. Kama kuna kifaa maalum au njia ya asili ya uhakika..

Pili, namna gani naweza kuhifadhi maziwa kwa muda mrefu yasigande pasipo kuyachemsha?

Shukurani zinatangulizwa wakuu!

kugundua maziwa kama yana maji tumia HYDROMETER ni chombo unaweka kinaelea kipo ambacho ni special kwa maziwa tu na vipo vya kawaida ili mradi kiwe na range ya uzito wa maziwa halisi,, Kwa KUTUNZA Chemsha yapooze kwa ghafla moja kwa moja weka kwenye fridge ubalidi unaokaribra kugandisha yasigande.

Zingatia mm ni mtoto wa mfugaji tu SIO mtaalam ... Tafuta wataalam wa maziwa hivi majuzi tu this year nasikia pana technology mpya ya maziwa hata mm sijaifahamu..
 
Natanguliza heshimu,
Mara zote huwa naamini katika intelligency ya baadhi ya wana JF. Ushauri tunaopata hapa umetusaidia wengi kwa namna moja au nyingine.

Ndg zangu, leo naomba nishauriwe namna ya kutambua maziwa yaliyochakachuliwa, yaani yenye maji. Maana mengine sio rahisi kuyagundua. Kama kuna kifaa maalum au njia ya asili ya uhakika..

Pili, namna gani naweza kuhifadhi maziwa kwa muda mrefu yasigande pasipo kuyachemsha?

Shukurani zinatangulizwa wakuu!
Japo nimechelewa saana kukupa ushauri wangu lakini naimani utakufikia.Kwanza Cha msingi tambua kuwa ng'ombe wote wanatofautiana, hawafanani Kama vile tunavyoelewa, huo ndio ukweli. Hivyo hata maziwa yao yanatofauti...

fano kuna ng'ombe anatoa maziwa mepesi wakati mwingine anatoa yaliyo mazito. Sasa utajuaje kama maziwa yameongezwa maji:chukua kiasi kidogo Cha maziwa Kisha mwaga chini juu ya ardhi, yenye maji yatapita haraka nakuzama ardhini huku yakiacha Alama kidogo ya maziwa wakati Yale mazito yatachukua muda kuzama na hayatazama yote mengine yatabaki juu as cream.

Pia unaweza chukua nguo km tisheti na ukaimwagia maziwa sehemu utagundua kuwa maziwa yenye maji hayataacha Alama ya rangi ya maziwa wakati Yale mazito yataacha Alama ya maziwa.

Au unaweza ukatumia lactometer ambayo ni kifaa Cha kupima uhalisia wa maziwa kwa kukuonyesha kiwango cha maji kwenye maziwa husika japo pekee hakitoshelezi kwa kuwa it works on principle of specific gravity ya maziwa hivyo ni lazima uongeze kuangalia fat content ndio uje upate overall composition kwa kuwa maziwa yanaundwa na vitu ambayo inaweza kuwa nyepesi au nzito kuliko maji yenyewe.
 
Back
Top Bottom