Naomba ushauri kuhusu biashara ya vifaa vya umeme

aliyetegwa

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
312
477
Wakuu habari,

Katika namna ya kuendelea kujitafuta nimekutana na wazo la kufanya biashara ya vifaa vya umeme vya majumbani kama bulbus, wire, main switches, zile pipe za kupitishia nyaya na vingine vinavyo husiana na umeme majumbani.

Naomba wanaojua walete michango yao, wagusie mtaji, faida na changamoto nyingine.

Natamani kufanya biashara hii kwa kuuza jumla na rejareja.

Natanguliza shukurani.
 
Ni biashara nzuri sana ...na inafaida sana hasa kwa rejareja ...mfano ukipata mteja wa kufunga wiring ya nyumba nzima...anakuachia kibunda kizuri tu chap

Changamoto kubwa ni wateja wako wakuu ni mafundi ...hivyo inabidi ujifunze namna ya kuishi nao...(sehemu zingine wanapewa % ya faida ) ..ili wazidi kukuletea wateja ...ukimudu hicho kitu ...utatoboa chap sana

Mtaji unaweza anza hata na 9M hata 6.5M unapata mali ya kutosha ...hapo ni nje ya vitu kama kodi ya kibanda ...TRA na leseni ya biashara


Faida kwa rejareja ni 30% ya mauzo..hiyo ni kwa maoeno yenye ushindani mkubwa ambapo bidhaa zinauzwa kwa bei ya chini ...ila inaweza kuwa zaidi ya hiyo ...all the best
 
Back
Top Bottom