Naomba kusaidiwa kuondokana na suicidal mindset

Korozoni

JF-Expert Member
Oct 24, 2016
264
105
Habari wana Jukwaa,

mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 25,nimesoma mpaka kidato cha sita lakini matokeo yangu hayakuwa mazuri.Mwaka niliofanya mtihani ni 2014.

Na baada ya matokeo kwenda mrama nilijitahidi kufanya kazi za hapa na pale ili nikusanye kiasi cha fedha kitakachoniwezesha kujiunga na vyuo vya kati.

Bahati mbaya sana pesa niliyoipata iliishia kuhudumia familia yangu(mimi,wadogo zangu na mama yangu),baba yupo na maisha yake pamoja na ndugu wengine ambao ni half brothers!

Kaka zangu(Half brothers) wamesoma kiasi chake na walikuwa wakitoa ahadi za kunisaidia kusoma lakini mwisho wa siku wanashindwa kutekeleza.

Hivyo nimekuwa nikiishi maisha magumu sana yenye misukosuko sana.

Lakini kuna jambo si jema lilianza mwezi desemba mwaka jana ambalo ni kujiwa na fikra mbaya kichwani zinazonishawishi kujiua kwa kujitupa mbele ya gari au kwa vitu vya ncha kali.

Hali hii ilianza mara baada ya tatizo la kichwa kuuma upande mmoja(migraines) kwisha.
Nimejaribu kulazimisha ubongo ufikirie mengine lakini wapi!naomba wataalam mliopo humu jukwaani mnisaidie nini hasa tatizo langu na nifanye nini kuondokana nalo,

Asante na nawasilisha!
 
Unadhani ni kwa nini unajisikia kujiua?
Yawezekana bado unamsongo wa mawazo kuhusu uliyopitia.
Waone washauri watakusaidia au nenda kaombewe, hiyo inaweza kuwa ni roho ya mauti.
 
Pole sana hali hiyo ilinipata kipindi Fulani hivi nilitamani kufanya hayo BT nilikuwa najipa moyo na kuamini mungu hakunileta duniani ili nipate shida sikupata msaada km wako kwa watu niliowategemea bt nilisimama nilipambana mpaka nijue hatma yangu sikuacha pia kulia na mungu na kumuomba kila siku mungu anajibu maombi usikate tamaa wewe mtoto wa kiume pambana one day utatoka usiruhusu hiyo hali
 
Hmmm!asante kwa ushauri,vipi huyo demu akianza kunipa stress zaidi?
Hii issue tulimsaidia mtu kama wewe ila msichana akipangwa na ndugu na watu wenye nia njema kabisa ila victim aliatempt kujiua kabisa alikunywa vidonge tukamuwahi
 
Pole sana mkuu kikubwa mwombe Mungu na jaribu kujichanganya na watu mbalimbali wa maeneo tofauti huwenda ukapata new idea kuhusu maisha au waweza safiri kutoka ulipo kwenda mkoa mwengine kuona watu wanaishi vp na changamoto zinazowakabili na vp wanakabiliana nazo huwenda ukabadili namna mawazo yako ya kushindwa yakabadilika na kujiamini kua you can do something which can change you life.
 
Habari wana Jukwaa,

mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 25,nimesoma mpaka kidato cha sita lakini matokeo yangu hayakuwa mazuri.Mwaka niliofanya mtihani ni 2014.

Na baada ya matokeo kwenda mrama nilijitahidi kufanya kazi za hapa na pale ili nikusanye kiasi cha fedha kitakachoniwezesha kujiunga na vyuo vya kati.

Bahati mbaya sana pesa niliyoipata iliishia kuhudumia familia yangu(mimi,wadogo zangu na mama yangu),baba yupo na maisha yake pamoja na ndugu wengine ambao ni half brothers!

Kaka zangu(Half brothers) wamesoma kiasi chake na walikuwa wakitoa ahadi za kunisaidia kusoma lakini mwisho wa siku wanashindwa kutekeleza.

Hivyo nimekuwa nikiishi maisha magumu sana yenye misukosuko sana.

Lakini kuna jambo si jema lilianza mwezi desemba mwaka jana ambalo ni kujiwa na fikra mbaya kichwani zinazonishawishi kujiua kwa kujitupa mbele ya gari au kwa vitu vya ncha kali.

Nimejaribu kulazimisha ubongo ufikirie mengine lakini wapi!naomba wataalam mliopo humu jukwaani mnisaidie nini hasa tatizo langu na nifanye nini kuondokana nalo,

Asante na nawasilisha!
We unadhan waliosoma mpaka degree wanapata ajira??
Kwa taarifa yako unauwezo wa kutosoa kuliko yoyote unaemdhania kafika degree ngap sjui

Kaa chini angalia akilini kwako ki2 gan unakiweza vzr zaid
Piga kaz mambo yatajipa2
 
Tatizo fikra hizo zinanijia involuntarily,sijui ni kwa sababu ya mawazo ya muda mrefu juu ya matatizo yangu?
 
hilotatizo nahisi ni mfadhaiko
hara Mimi ninao Ila sio wa kujiua..
Una miezi mi4 sasa
cha kufanya ni kujiamini, ondoa hofu na woga..
tafuta maana ya maisha las kuangalia mema ya dunia sio mabaya.
jipe moyo utashinda.
omba Mungu pia akusaidie kuepuka hayo.
halafu uyachukulie kawaida..
acha mitazamo hasi katika kilajambo.
pia unapoanza kuwa OK,usizirudie fikra zile tena. zitaanza upya
 
Mkuu fikiria watu wenye shida zaidi. ..tembelea watu tofauti in hospitals etc....ukiona watu wanastruggle zaidi n yet they keep moving huenda ikakusaidia kujikwamua upya+kukupa faraja.
 
Pole sana.

Jitahidi sana kuwa Karibu na Muumba wako.

Nikiwa na maana,

Jitahidi sana kufanya Ibada kwa Imani yako yoyote ile, itakusaidia.

Pia, kwa kila jambo lako lolote lile Mtangulize Muumba wako kwanza.

Pili,

Hebu jiangalie wewe Mwenyewe kwanza, na kisha waangalie wale ambao wewe ukiwaangalia unaona kabisa hali zao ni za chini zaidi kuliko wewe, amma naweza sema wale ambao umewazidi kwa chochote, ikiwemo:-

Afya, Hali ya Kimaisha, Kipato N.K, kisha jifananishe na wewe. Utagundua Mwenyezi Mungu anakupenda sana.

Wewe unalala ndani unawaza kujiua, kuna wenzio hawana hata pa kulala na hawafikirii kitu kama hicho.

Wewe una Macho yako yote mawili, Mikono yako yote miwili, nguvu unazo.

Kwanini uwe Mtu wa kukata tamaa?

Jitahidi kujifunza kuyazoea Maisha kwa Hali yoyote ile utakayokumbana nayo, na usipende kujifananisha Maisha yako na yale Maisha ya waliokuzidi.

Muhimu kuwa na Moyo wa Ghadhabu, niamini, ipo Siku utatoka tu.

Kila unaemuona kwenye Maisha ana Viama vyake, au kuna Viama alivipitia/alishavipitia, ila wewe hujui/hufahamu

Hakuna Maisha rahisi.

Wewe gangamala
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom