Naomba kuongea na wewe kwa maandishi

Naomba kuongea na wewe kwa maandishi

love more than100

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2014
Posts
2,061
Reaction score
715
JE, FEDHA ZAKO ZA BANK ZIPO SALAMA?

Jamani imenitokea mimi na hivyo iwe fundisho, angalizo na umakini kwa wengine. Account zetu za Bank hazipo salama hata kidogo. Majuzi nikiwa nimepozi na ndugu zangu huku tukiwa tunapata kinywaji, na Wenzetu maeneo mengine ya nchi wakisheherekea sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, niliamua kwenda Bank kuchukua vijisenti kidogo. Nikiwa ndani ya chumba cha ATM pale sheli Total Mlimani City nilichomeka kadi yangu na kutaka kutoa fedha kwenye account yangu ya NBC.

ATM machine iliashiria ya kwamba sikuwa na kiwango cha fedha cha kutosha kuweza kukamilisha muamala unaozidi 100,000/-. Nilipaswa kuchukua kiwango kuanzia 50,000/- kwenda chini! Nilishtuka kwakweli. Account yangu ilikuwa na Uwezo wa kunipa muamala mkubwa zaidi. Yaani hata zaidi ya 400,000/- ambayo ni Maximum kwa ATM.

Niliamua kwenda Mlimani City kabisa. Yale yale yalijirudia. Nikaamua kutoa 50,000/- huku nikijifariji ni tatizo la kimtandao maana nilijaribu ATM za CRDB pale nje zikaonesha zipo out of service! Lakini wakati natoa hizo pesa niliomba statement ambayo ilionesha kiwango Kikubwa cha pesa hakipo! Nikajumuika na jamaa zangu huku nikiwahoji kwa kile kilichonikuta. Tukapeana moyo leo niende Bank ya NBC kuhakikisha.

Sikupata usingizi. Asubuhi ikawaidia. Nikaingia tena kwenye ATM kuthibitisha na kujiridhisha kama kweli ulikuwa ni mtandao. Nikakuta salio langu limepungua zaidi.

Nasukuma milango mizito ya pale NBC Mlimani City. Nikaomba statement manually. Zikawa zimepungua tena. Yani mwendo wa kutoka kwenye ATM hadi ndani pesa zilitolewa /ibwa. Dada au customer care aliyekuwa pale akaniambia mbona inaonekana nime swap card Nakumat Supermarket?! Nilishtuka maana sikuwahi ku swap card popote pale toka nizaliwe.

Lakini alipoangalia vizuri akagundua card imekuwa swaped kwenye Nakumat ya Nairobi. Nayeye akastuka. Akaniambia kaka subiri kuna tatatizo. Nikamuomba Bank statement ya miezi 2. Yaani December-2014 na January 2015. Sikuamini nilichokutana nacho. Account yangu nimekuta imeibiwa zaidi ya Tsh Million 6.

Transactions zote zimefanyika Nairobi, Kenya. Wizi huo umeanza kufanyika toka-December 20, 2014. Na sehemu kubwa ni kwenye Nakumat Supermarket. Walichoniambia NBC nijaze claim form na kuandika barua. Nimefanya hivyo. Nasubiri majibu yao. Hata hivyo wakati najaza form nilikutana na watu kadhaa wakiwa nao wameibiwa kwa mfumo huu huu.

Hivyo ndugu zangu, kwa wenye account za NBC wakazikague. Waulize Bank statement. Bank hii siyo salama tena. Nilipata msg ya Wizi huu wa Fedha last year December nikapuuzia. Na bank husika ilitutumia msg wateja wake kwamba habari za Wizi wa mtandao zilikuwa za uzushi tu! Leo nimeamini haukuwa uzushi. Pesa zinaibwa. Angalieni account zenu zote na isiwe NBC tu.

Nawatakia siku njema. Hayo ndiyo yaliyonikuta yatima mie hapa Sina hamu but bank wanasolve kunirejeshea but itakuwa lini sijui.
 
JE, FEDHA ZAKO ZA BANK ZIPO SALAMA?!

Nawatakia siku njema. Hayo ndiyo yaliyonikuta yatima mie hapa Sina hamu but bank wanasolve kunirejeshea but itakuwa lini sijui!

Duuu! It is a shock! Pole mdada. But imekuwa njema umegundua mapema. Hata ivo, pesa yako bank iko salama. Ukishapeleka pesa bank, tayari ile ni mali ya bank. Ikiwa ni cyber theft imetokea....bank hiyo itakupa pesa yako pasi na shaka. Ila cjui ndo inachukua muda gani kuirejesha hela iliyo ibiwa...but cna shaka ni ktk muda sifuri pesa yako ipo kama ulivoweka. NI JUKUMU LA BANK KUBAINI mbinu zozote za wezi wa pesa na KUBUNI mbinu za kuzuia wizi usiwepo. HAKUNA MAHALI PENGINE PALIPO SALAMA KUTUNZA PESA YAKO...ISIPOKUWA BANK. Xo, keep trusting the bank. Hata kama bank ikiungua.....pesa yako ipo.
 
Okay!! Bank za Bongo sio salama, no wonder watu wanakimbiza pesa zao New Jersey au Cayman!!
 
Yaani kanishtua hatariii.
Jana tu nimetoka kuingiza mpunga NBC.
Ngoja nihamie mkombozi

Haaaa ukataka ukahamishe mpunga fasta... ni ya siku nyingi nilitumiwaga katika group whatsup
 
Yeye Appuch amesema ilimtokea siku ya maadhimisho ya mapinduzi ya Zanzibar, 12/01/2015, kama nae ametunga hadithi basi ni uzushi uliopindukia. Kuna vita kubwa ya kuibia wateja kati ya bank za CRDB na NBC.
 
Last edited by a moderator:

NAKUKOSOA mkuu Bigurube. Mim cjasema kuwa ilinitokea mim. Me nimem- quote mkuu Love more than 100, katika thread yake "NATAKA KUSEMA NA WEW KWA NJIA YA MAANDISHI". Love more than 100ndo yalimkuta. Mim nime-comment tuu. BANK NI MAHALI SALAMA KUWEKA PESA YAKO...Hili halibadilishwi ni iyo cyber theft ilomtokea love more than 100 na mwingne yeyote. Pesa yako iweke bank na itakuwa salama...hayo malalamiko yapo tuu, lakn pesa yako bank itakupatia. Fuata taratibu tuuu.
 
Ok am sorry bwana c unajua hii ni Blue Monday, hata mm bado naamini kuwa bank ndipo mahali pekee pa kuhifadhi senti zetu, hata km zitapotea si juu yetu ingawa inaleta usumbufu kwa kipindi kile unspokuwa unafuatilia na hasa km una account moja pekee!
 
Ouph! Is it Monday again? Worry out, nafurah tu ukielewa kwa usahihi. Don't get up-set of Mondy, nothin new on it.
 
Back
Top Bottom