Naomba kujuzwa utaratibu wa kupata mbegu ya swala

Samson Ngomboli

JF-Expert Member
Oct 30, 2019
1,428
2,241
Nawasalimu wanaJF wote,

Najua JF ina watu wa kila taasisi na idara. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba kujuzwa utaratibu wa kupata mbegu za wanyama kama swala na digidigi maana siku za karibuni Rais amesikika akisisitiza uwepo wa mapunguzo ya bei ya wanyama pori kwa ajili ya kuwafuga mathalani swala kutoka dollar 150 mpaka elfu sabini n.k.

Hivyo mwenye kujua chochote atujuze tafadhari ili tuchangamkie fursa za kufuga.

Nawasilisha.
 
Mkuu kwa sheria zetu kumbe inawezekana kununua mnyama pori ukafuga kwa biashara? Iko vizuri mwenye uelewa afafanue hili tafadhal.
Nilimsikia Rais akisema wamepunguza bei ya wanyama pori mfano swala 70000, nyati laki Saba n.k. na akawa anawasisitiza watu wanunue wafuge ili baadae kuwepo hata na bucha za wanyama pori,ndio maana naendelea kuwasubilia wajuvi watujuze.
 
We muache ajiingize mkenge limkimbize mpaka mtaa wa pili mpaka wamwitwa wanyama pori unafikir wazo la kumfuga watu wa kale walikuwa hawana walishindwa
Kuna sehemu barabarani kabla ya kuingia Mwz kuna kituo cha serikali cha hizi mambo za mifugo,niliona hybrid ya Nyati na ng'ombe wa kawaida,sijajua walizalishwa vile kwa malengo gani labda ni majaribio/nyama/maziwa lkn niliona wako poa.
 
Kuna sehemu barabarani kabla ya kuingia Mwz kuna kituo cha serikali cha hizi mambo za mifugo,niliona hybrid ya Nyati na ng'ombe wa kawaida,sijajua walizalishwa vile kwa malengo gani labda ni majaribio/nyama/maziwa lkn niliona wako poa.
Mara nyingi ni majaribio ya kisayansi ila siku zote species mbili zikizaa jua kiumbe atakayekuja hawez kuzaa ni km final so hybrid ni msosi tu hawawez kuzaa.
 
Back
Top Bottom