Naomba kujuzwa mbadala wa kisimbuzi cha DStv

iCode

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
758
439
Habari za muda huu wakuu,

Naomba msaada wenu, nahitaji kuacha kitumia king'amuzi cha DStv kwa sababu ya kupandisha gharama zao kila siku, yaani hawatabiriki.

Naamini wengi tupo kwenye hii kadhia kwa sasa. Penye wengi pana mengi, karibuni tusaidiane alternatives.
 
Kumbe na wewe msg umepokea msg toka kwao, na mimi nimepokea nikawaza kuwahama ila sioni mbadala itabidi nikomae nao tu japo mimi si mpenzi sana wa TV maana kila ntakacho asilimia 90 ntakipata mtandaoni
 
Habari za muda huu wakuu,

Naomba msaada wenu, nahitaji kuacha kitumia king'amuzi cha DStv kwa sababu ya kupandisha gharama zao kila siku, yaani hawatabiriki.

Naamini wengi tupo kwenye hii kadhia kwa sasa. Penye wengi pana mengi, karibuni tusaidiane alternatives.
Hakuna mbadala wa DStv ila DStv ndio mbadala wa kila aina nyingine za visimbuzi.
 
Hapo mtaani kwako hakuna cable tv za wahindi? Kama zipo basi ndio mbadala wa DStv, vuta cable ufurahie maisha kwa elfu 15 tu kwa mwezi.
 
Dawa ni kuachana NAO sasa! Movie ya 19 kweusi ndo wanarudia kila leo.

Zaidi ya Soccer, hamna jingine! Sasa kulipia hivyo vifurushi wa soccer tuwaachie wenye Bar na kumbi za kuonesha mpira, sisi tukajazane huko kwa buku tu!
 
Mm nilikuwa na mpango wa kuwapiga chini ila shida ni watoto wangu wameizoea sana, kuna cartoon nyingi ambazo wanazipenda sidhani kama huko kwingine watazipata. Hawa jamaa kwenye compact walikuwa 44k wakaja 49k wakenda 56k sasa wameingia 60k ndani kama ya miaka miwili hivi. Ukiangalia hili ongezeo ni kubwa kwa huu muda mfupi basi tu tunachulia poa, alafu bado wanakunyima Uefa Champions League
 
Back
Top Bottom