Ni zoezi gumu, ila ukijipa muda unafanikiwa.Unaandika tweet nzuri kuhusu nini?
Je umekuwa na ubora wa juu kabisa katika unachoandika,kama bado ongeza bidii...na usiwe unahama hama mada zako, kama ni sports and gamea basi concentrate hapo na uwe fasta sana kupost kabla habari haijawa viral, sio leo sports baadae kidogo politics.
Tumia hashtags zinazohusika.
Weka picha zenye resolution nzuri.
Tweet muda ule ule kila siku mfano tweet ya kwanza saa moja na nusu asubuhi, ya pili saa saba kamili mchana na ya mwisho saa mbili au nne usiku.
Washa notification kwa baadhi ya kurasa kubwa za suala kama lako kama ni mpira labda goal dot com, wakipost, tafsiri ile habari weka kwako pia retweet mapema sana,ili uwe ahead of time.Ukitweet 3-5 per day kwa siku 365,hata algorith ya tweet itaanza kuku favour.
Mwisho kumbuka hakuna njia ya uhakika asilimia mia.