Naomba kujuzwa jinsi ya kupata followers laki 1 kwenye mtandao wa Twitter

stivii

Senior Member
Nov 5, 2013
171
225
Habari wadau,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mimi ni mtumiaji wa mtandao wa twitter toka mwaka 2015 lakini mpaka sasa nimefanikiwa kuwa na followers 500+.

Kwa mujibu wa wadau, followers wa twitter ni hela kuna namna mbalimbali ya kuingiza pesa kwa kutumia mtandao wa twitter lakini kigezo kikubwa lazima uwe na namba kubwa ya followers.

So, naomba mnisaidie wadau namna ninavyoweza kupata followers laki moja kwa muda mfupi maana nataka kuwa influencer ili nipate matangazo au kuuza bidhaa.

Nimekuwa najaribu kuandika tweet nzuri lakini zinakosa wasomaji na followers bado hawaongezeki.

Najua siwezi kukosa wataalamu wakanisaidia njia mbalimbali.

Asanteni.
 
Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
1,149
2,000
Kama ni kuuza bidhaa sio lazima uwe na organic followers wengi, tumia matangazo ya kulipia kulazimisha wasio followers wako waone bidhaa zako.
 
Drat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
683
1,000
Ni zoezi gumu, ila ukijipa muda unafanikiwa.Unaandika tweet nzuri kuhusu nini?
Je umekuwa na ubora wa juu kabisa katika unachoandika,kama bado ongeza bidii...na usiwe unahama hama mada zako, kama ni sports and gamea basi concentrate hapo na uwe fasta sana kupost kabla habari haijawa viral, sio leo sports baadae kidogo politics.
Tumia hashtags zinazohusika.
Weka picha zenye resolution nzuri.
Tweet muda ule ule kila siku mfano tweet ya kwanza saa moja na nusu asubuhi, ya pili saa saba kamili mchana na ya mwisho saa mbili au nne usiku.
Washa notification kwa baadhi ya kurasa kubwa za suala kama lako kama ni mpira labda goal dot com, wakipost, tafsiri ile habari weka kwako pia retweet mapema sana,ili uwe ahead of time.Ukitweet 3-5 per day kwa siku 365,hata algorith ya tweet itaanza kuku favour.
Mwisho kumbuka hakuna njia ya uhakika asilimia mia.
 
Ngareroo

JF-Expert Member
Aug 11, 2019
1,810

Ushauri mzuri sana bro
 
walosie

Member
Dec 13, 2018
19
45
Anayehitajii njia rahisi ya kupata followers twitter nichek 0745187765 whatsap

Kuandika huku naona itachukua page 278
 
PabbyMontana

Member
Jun 27, 2014
99
225
Anayehitajii njia rahisi ya kupata followers twitter nichek 0745187765 whatsap

Kuandika huku naona itachukua page 278
Kwanini usiandike hapa maana swali limeilizwa hapa kwa faida ya wwngi.

Haya mambo ya kufwatana inbox au kumwambia mtu apige simu umuelekeze ni dalili za utapeli.

Kama kuna malipo inabidi ulipwe ili uelekeze then be straight sema hapa ueleweke.

Mambo ya njoo in-box, mara nicheki kwa namba hii ni ya kizamani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom