Naomba kujulishwa kwa sababu za kitaalam; Ipi nyumba bora kati ya tofali za kuchoma na cement?

Leo nimepita maeneo ya SHABAHA Moshi leo nikaona nyumba zote ni tofari za kuchoma,je ubaora wake ni upi ukilinganisha na tofari ya cement?
Matofari ya kuchoma ni Imara zaidi kuliko ya cement, hata ikitokea nyumba imeungua moto, nyumbani tofari za cement itakuwa haifai tena kwa asilimia kubwa hasa kama imeungua kwenye kuta,wakati za kuchoma inakuwa ndo zimeimarishwa zaidi na ule moto...
 
Nafikiri za kuchima au zile za tope kabisa ambazo hazijachomwa ni bora kuliko za cement, kisayansi ya mtaani isiyokua rasmi ni kwamba, cement inatengenezwa kwa chemicals na zinamuda wa kuisha nguvu zake kadri muda unavyosogea, cement life span yake ni ndogo kulinganisha na tofali ya udongo.

Kingine ubora wa tofali ya cement unavigezo vingi mfano ratio ya mchanga na cement, aina ya maji, kiasi cha umwagiliaji wa tofali baada ya kufyatuliwa na ubora wa vifaa vinavyotumika.

Hali kadhalika tofali za kuchoma ziive vizuri ili kuongeza ubora.
 
Halafu tofari za kuchoma zinafaa kujengea msingi kwenye maeneo ya magadi?
 
Peleka maabara kufanya vipimo baada ya hapo utuletee majibu kwa njia ya picha,tutajua lipi bora n lipi bora zaidi
 
Back
Top Bottom