Mr Antidote
JF-Expert Member
- Jan 11, 2015
- 944
- 1,271
Habari zenu wana JF,
Kuna kitu nimekiwaza na kukitafakari kwa muda wa kama siku 3 hivi lakini bado sijapata majibu yake. Basi nipo hapa kuomba msaada wa kueleweshwa kiundani kwa watu wenye uelewa wa mambo ya kidini awe muislam, mkristo budhaa na hata asiye na dini.
Suala kubwa linalonitatiza ni kuhusu ukweli wa siku ya kiama, jehanamu na pepo. Je kweli hivi vitu vipo kweli? Nikiri wazi kabisa kwamba mimi ni mkristo mkatoliki na nimekua nikifundishwa haya kama sio kukaririshwa toka nikiwa mdogo katika mafundisho ya komunio ya kwanza na kipaimara kwamba kuna hivyo vitu 3 nilivyovitaja.
Yafuatayo ni maswali ambayo najiuliza na ningefurah kama nitapata majibu ya kina na kuridhisha.
1. Je ni kweli kuna siku ya kiama?
2. Na kama kweli ipo kwanini MUNGU aliwaadhibu na kuviangamiza baadhi ya vizazi kwa matendo yao machafu na kutosubiri siku ya kiama?
3. Je hawa walioadhibiwa na kuangamizwa siku za nyuma walikuwa waovu kuliko sisi wa zama hizi?
4. Je hao walioangamizwa wataletwa tena mbele ya hukumu? Na nini hatima yao na ilihali walishaadhibiwa kwa kuangamizwa?
Baada ya kupata ufafanuzi wa kutosha wa maswali hayo nadhani suala la pepo na jehanamu nitaweza kulielewa kwa urahisi.
Inawezekana kabisa kuwa kuna mada kama hii imeshawahi kujadiliwa kama hamtojali naomba kuwekewa link yake.
NB: Nimetumia zama za nabii Nuhu na gharika kuu kuuliza maswali hayo.
Shukrani.