Mkuu kuhusu kuhack whatsapp kuna vitu inabidi uelewe. Kwanza unahack kwa njia gani na wapi.
1)Njia ya kwanza ni kuhack kwa kuingilia transmission ya message kutoka kwa sender na receiver kisha wewe ukazisoma. Hii haiwezi kufanikiwa bila kubreak encrption na wameiziba hii kwa kutumia hio END TO END encryption so hacker au mzamiaji yyt yule hawezi kuingilia calls au sms zozote kwa hii njia.
2)Njia ya pili ni kusubiri sms zitumwe kisha zikae kwenye simu ya mtumiaji na hacker azibebe kutoka kwenye hio simu(Kumbuka sms za whatsapp zinatunzwa kwenye simu ya mtumiaji, sio kama telegram ambapo zinatunzwa kwenye database ya telegram). Hii njia ya pili ndio ambayo bado whatsapp hawana mbinu efficient za kuizuia. Na njia zote za kuhack mawasiliano ya whatsapp zilizoonesha mafanikio zimebase kwenye msingi huu. Kwa maboresho yaliyofanywa na whatsapp miaka ya hivi karibuni yameweza kuzuia hii njia kwa kiwango fln lkn gurus wa hacking bado wana njia zao wanazotumia.
Nitakupa mfano kutoka kwa NSO group ambalo ni israeli based cybersec company lililodaiwa kutengeneza technology ilotumika kudukua mawasiliano ya Jeff Bezos(richest person on earth) mwaka 2019. (soma habari hio hapa
Jeff Bezos Hacked By Prince of Saudi arabia)
Hawa jamaa NSO wanatengeneza sms fln ambazo zinakua ni scripted kwa maana kwamba zikiingia kwenye simu ya mtumiaji zitaonekena kama sms lkn app ya whatsapp ikiziingiza kwenye message store zinageuka kuwa kama programs fln(scripts) ambazo zitacommand simu iupload sms zote kutoka kwenye message store including all keys. Hizi data zikienda kwa hacker ndipo anapoweza kusoma sms zako zote. Kwa Jeff Bezos inasemekana alitumiwa picha ya mke wake wa zamani na Prince wa Saudi Arabia, na hio picha ndio ilitumika kudukua mawasiliano uake.
Pia NSO Group ilishawahi kushtakiwa na whatsapp kwa kudukua mawasiliano ya watu mbali mbali, waweza soma habari hio hapa
Whasapp sues NSO Group
So kama unavyosema serikali inaweza kusoma sms zako endapo tu wanaweza pata hio technology ya kudownload sms za whatsapp kutoka kwenye simu ya mtumiaji lkn kama wanainter-cept mawasiliano basi hio ni ngumu coz tyr end to end encryption imeshaziba hio kitu.
Kuna wakati NSO Group ilisema kwamba wao hupokea orders kutoka kwa serikali mbalimbali na Security agencies ili kufatilia mawasiliano ya targeted people japo sikumbuki source ya hii habari so dont take it serious.