Naomba kujua sheria za kiujumla za ujenzi

UZZIMMA

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
406
456
Habari zenu humu ndani. Jamani mimi naomba msaada wa kujua general specification za sheria za ujenzi.
Aidha nipewe ufafanuzi au nirushiwe document kama pdf iliyosheheni sheria za ujenzi.

Miongoni mwa mambo hayo ni umbali unaoruhusiwa l kutoka barabara kuu, jinsi gani ya kutumia mipaka ya ujenzi. Umbali unaoruhusiwa kutoka vyanzo vya maji, na kadhalika.

Nikisaidiwa hilo nitashukuru sana.
 
Ukitaka kujua mambo hayo vizuri kachukue diploma/bachelor degree ya ujenzi.
 
Ahahahahhaha . Wewe jenga tu nyumba ya ndoto yako .
Popote pale cha msingi uwe mwanachama wa mbogamboga.
Manispaa na halmashauri ndio hutoa vibali vya ujenzi. Nenda huko
 
Kama barabara ni ya TANROAD sheria mpya ni 22.5m kutoka katikati ya barabara.
Sheria ya zamani ni mita 12.5 kutoka katikati ya barabara.

Sheria za barabara za mtaani nadhani we toka mita 6 toka katikati ya barabara hii ina maana utaacha sehemu ya kuchimba mtaro na barabara pia. (Not sure kuhusu mita)

Sheria ya vyanzo vya maji ni mita 60 toka chanzo cha maji kinapoishia.
 
Back
Top Bottom