Naomba kujua mishahara, posho, mafao na kodi wanazokatwa wabunge kwa mapato hayo

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Wadau Nawasalimu,

Naomba kujua mishahara posho na mafao wayapatayo wabunge wetu. Sambamba na hilo, naomba kujua kodi wanazokatwa kwenye mishahara posho na mafao yao.
 
Jumla ya mshahara na mapochopocho mengine, ni Milioni 12 kwa mwezi.

Hapo ni nje na zile posho za vikao wakati Bunge linaendelea! Ukiteuliwa kuwa Mheshimiwa Waziri, posho zinaongezeka tena. Sihasa nivtamu sana. Sifa kuu ya kujiunga ni; kujua tu kusoma na kuandika.

Kila baada ya miaka 5 anakabidhiwa kiinua mgongo cha Tsh. Milioni 300 hivi! Na mzigo wote unawekwa kwenye akaunti. Hawa wateule wetu hawahusiki na kile kikokotoo cha 33%!!

Maana wenyewe wana akili nyingi za kutunza fedha zao, ukilinganisha na wale watumishi wa umma ambao wanaaminika eti hawana uwezo wa kutunza vile vimilioni 60 vyao walivyo vihangaikia kwa miaka zaidi ya 30 ya utumishi wao! Ndiyo maana serikali yao sikivu imeamua kuwatunzia kwa lazima.

Hao waheshimiwa wana sifa ya kukopa mpaka milioni 600 benki kutokana na uheshimiwa wao!! Mungu awape nini tena!! Gunia la chawa wajikune?
 
Mshahara 12m per month, sitting allowance 350,000per day, house allowance 2m, electricity and water 1m, pia mshahara Hauna PAYE, Mkopo 200m Hauna riba, plus 500m akimaliza 5yrs, kama kiinua mgongo, Ila kwakua Kuna tozo mpya zimekuja hope washaongezewa mshahara na posho, so tuendelee kubuni tozo zingine ili wabunge wetu waweze kulipwa walau 30m per months.
 
Asante kwa Majibu Mazuri VIPI Suala la KODI wanazokatwa?
 
Back
Top Bottom