Nitakupa maana yangu niliyoibuni nilipokuwa mdogo chini ya miaka 10. Nilimuuliza Bibi yangu mzaa Baba: Sisi tumeumbwa na Mungu. Je, Mungu aliumbwa na nani? Mungu alitoka wapi? Na kama hakuna Mungu ndo maana hakuna kitu, kila kitu hakuna kabisa ni utupu (empty) nikaingia ndani nikazama peke yangu nakuambia nilikalibia kuchanganyikiwa. Ebu na wewe waza kama nilivyowaza hata sasa hivi kwamba kama hakuna asili ambayo hiyo asili ilipelekea wewe kuwako na fikilia kwa vile kila kitu kina mwanzo fikilia kuwa mwanzo haupo zama ndani baba/mama hawakuwahi kuwako na wewe automatically usingekuwepo nenda backwards ndani nakuambia utafikia kuchanganyikiwa. Sasa hiyo asili ambayo ukitaka kuiondoa unapelekea ubongo kuchanganyikiwa ndo Mungu. Mungu ndo asili ya kila kitu! Mungu alikuwepo! Ilikuwaje akawepo hakuna hajuaye na ukitaka kumuondoa na kuamini hayupo automatically utachanganyikiwa. Kitu cha kwanza kuumba ulikuwa muda. Muda uliumbwa kwasababu Mungu haishi kulingana na muda. Mungu uishi katika umilele. Kwahiyo uumbaji wote ulianza pale alipoumba muda. Huu muda tunaoujua kwa sekunde, dakika, saa, siku, wiki, mwezi, mwaka, majira, nyakati, n.k. viliumbwa. Fuatilia mwanasayansi anaitwe Stephen Hawking' Anakubali kuwa kitu cha kwanza kuumbwa ni Muda na kwamba Mungu hayupo kwasababu angekuwepo angetakiwa kuwa na muda (time) ya kuumba muda na kwamba muda ulijiumba automatically (big bang). Nahitimisha kwa kusema: Aliyeumba muda ndo Mungu kuanzia pale akaumba kila kitu tukiwemo wanadamu