Naomba kujua maana neno ya TRAINEE

SONGEA

Senior Member
May 29, 2008
101
8
Wanajamvi naomba msaada wenu kunifahamisha maana ya neno TRAINEE.

Nauliza hilo baada ya kuona kwenye kampuni ninayofanyia kazi NO matangazo ya kazi wala michakato ya ajira. Badala yake kila siku anakuja mtu eti ni trainee. Hata ambapo. Binafisi naona hii inahatarisha ajira zawatu, maana mtu akienda likizo siku inayofuata analetwa mtu eti ni trainee. mwenyewe akirudi basi wanaendelea kufanyakazi wote. Usalalma wa kazi kwa huyu mtu uko wapi?

Mbaya zaidi ni pale inapobainika kuwa kuna mpango wa kuwapeleka short course hawa trainee. Je, hili neno limetumika vizuri ndugu zangu??
 
Una elimu kiwango gani wewe? maana hata darasa la tatu angeangalia katika kamusi na pia hao wanapata ujuzi kama wewe ulivyopata. Kama ulisoma shule unapomaliza huwezi kujua kufanya kazi ndio maana ukaanzishwa mfumo wa SEAP kwa mainjinia, madaktari n.k. Mwisho huku jf ni great thinkers kama vipi kapoteze muda huko fb
 
Trainee ni mtu aliye kwenye mafunzo ya kazi husika, kwa ujumla mtu huyu ni mwajiriwa ila cheo chake hufuatwa na neno trainee kwa mfano, manager trainee, operator trainee, chief technician trainee n.k. Baada ya muda neno trainee hufutwa baada ya kubainika kuwa sasa ameiva. Kipindi cha u-trainee mtu hufanya kazi chini ya watu fulani ambao humwangalia utendaji wake.....

Hope itasaidia......
 
Una elimu kiwango gani wewe? maana hata darasa la tatu angeangalia katika kamusi na pia hao wanapata ujuzi kama wewe ulivyopata. Kama ulisoma shule unapomaliza huwezi kujua kufanya kazi ndio maana ukaanzishwa mfumo wa SEAP kwa mainjinia, madaktari n.k. Mwisho huku jf ni great thinkers kama vipi kapoteze muda huko fb

Nakushukuru mkuu. Si kwamba nataka kufanyakzi peke yangu. Ila tatizo ni pale ambapo unakuta hakuna mchakato wa wazi wa ajira. From no where, mtu anapita ofini anamtambylisha, ..... huyu ni (JINA) ni (position) traiinee.

Mfano live: HRO aliacha kazi. Baada ya miezi 4 akaletwa mtu kwamba ni HRO trainee. Hakuna mchakato wa wazi ulioonekana. Tatizo langu si kuitwa trainee, ila huyu mtu anakuwa trained na nani maana HRO ka sasa hayupo. Na hii ni katika shirika la Umma
 
Inaonekana wanatoa kazi kwa kujuana na hawafati sheria za ajira...na huo ndio mwanzo wa kuwa kibaraka wa mtu aliyekuleta kama ni dada utaombwa ngono kama malipo ya kuwekwa kazini kama ni kaka utaishia kuwa kuwadi au watchman wa aliyekuleta.
 
Kama mdau ulivyosumbuliwa na hili neno hata mimi pia lilinisumbua sana kipindi fulani! Maana yake halisi ni mtu ambae ameajiriwa katika nafasi fulani na hana uzoefu nayo kwa maana kwamba hajawahi kuifanya na kwa kawaida huwa chini ya uangalizi wa mtu mwenye uzoefu kitaalamu huitwa apprenticeship training. Hata hivyo waajiri wengi wajanja wajanja wamekuwa wakilitumia kama fimbo ya unyonyaji na kupeana ajira kwa mfumo wa kujuana juana hivi. Kwa Tanzania hakuna sheria inayotambua hiyo nafasi.
 
Wanajamvi naomba msaada wenu kunifahamisha maana ya neno TRAINEE.

Nauliza hilo baada ya kuona kwenye kampuni ninayofanyia kazi NO matangazo ya kazi wala michakato ya ajira. Badala yake kila siku anakuja mtu eti ni trainee. Hata ambapo. Binafisi naona hii inahatarisha ajira zawatu, maana mtu akienda likizo siku inayofuata analetwa mtu eti ni trainee. mwenyewe akirudi basi wanaendelea kufanyakazi wote. Usalalma wa kazi kwa huyu mtu uko wapi?

Mbaya zaidi ni pale inapobainika kuwa kuna mpango wa kuwapeleka short course hawa trainee. Je, hili neno limetumika vizuri ndugu zangu??

trainee means under instruction,nikama mtu anapofundishwa gari anaendesha akiwa namtu pembeni ambaye ni mtaalamu wa kuendesha akimpa maelekezo pale inapo bidi,akizoea anaanza kuemdesha akiwa mwenyewe.kuhusa swala la usalama wa ajira za hao jamaa acha uoga,mtu kuletwa kwenye kitengo chako inawezekana kampuni inakua ingependa kua na watu wawili kwa hiyo post,usiwe muoga jambo la msingi monitor your perfomance.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom