Naomba kujua kuhusu mkoa wa Njombe

Wgr30

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
1,770
2,375
Salaam wanaJf,

Mwishoni mwa wiki hii nina safari ya kwenda mkoa wa Njombe nitakuwa huko kwa mda mrefu kidogo, kwa hiyo naenda kuanza makazi mapya natokea mwanza, sijawahi kufika huko.

Natamani/napenda kujua usafiri wa kutoka mwanza hadi huko kwanza ni gari ipi inayofika huko na ubora wa gari lenyewe, barabara ikoje kwa sababu nitakuwa na mizigo ambayo ikipata barabara mbaya inaweza isifike ikiwa salama, Ni masaa mangapi kutoka mwanza hadi huko,

Hali ya hewa ikoje, watu wake je! vipi kuhusu upatikanaji wa maji, maisha yakoje huko? upatikanaji wa nyumba za kuishi gharama zikoje?

Msaada wenu wakuu naamini humu kuna wenyeji wazaliwa na wakazi wa huko!

.........................

Wakuu tayari niko mkoa wa Njombe

Kiukweli baridi huku sio ya kuuliza kwa watu tuliozoea kuishi mikoa ambayo haina baridi huku utapata shida sana ikiwa ni pamoja na mimi kwa sasa shida ninayopitia ni baridi aisee!!

Kati ya watu 10 9 wana makoti au asiwepo kabisa ambaye hana koti tena koti haswaa!

Huko ni milima na mabonde sehemu tambalale ni chache sana!

Kuna sehemu unapita kutokea makambako kuna shamba la chai Eneo kubwa sana kwambele kidogo utaona kampuni inayolimiliki shamba hilo inaitwa KIBENA sijui kama nimepatia hilo jina.

Wabinti wazuri/warembo huku ni changamoto kiukweli (ukweli mchungu)

Watu wajombe wanajitahidi sana kwa usafi, maeneo mengi ni safi sana!

Nyumba za kulala/Guest ni nyingi sana!

Nyumba za huku zimeezekwa kwa mabati ya zamani sana nadhani zimejengwa zamani!

Ni mengi mazuri wakuu mazuri na mabaya pia!
 
Kufika njombe ni siku mbili chukua gari ya kutoka mwanza adi mbeya ambayo itakufikisha mida ya saa moja hivi usiku ukipanda asubuh SAA kumi na mbili utashukia makambako ambapo utapanda gari nyingne ya kukufikisha njombe na pia andaa makoti mablanket ya kutosha sababu kuna bardi Kali San na watu wa huko ni wakarmu tu karbu nyanda za juu mkuu.
 
Kufika njombe ni siku mbili chukua gari ya kutoka mwanza adi mbeya ambayo itakufikisha mida ya SAA moja hivi usiku ukipanda asubuh SAA kumi na mbili utashukia makambako ambapo utapanda gari nyingne ya kukufikisha njombe na pia andaa makoti mablanket ya kutosha sababu kuna bardi Kali San na watu wa huko ni wakarmu tu karbu nyanda za juu mkuu
Mkuu, kwanini asipande basi la Mbeya-Songea akashuke Njombe moja kwa moja? Nadhani itakuwa vyema akipanda la kwenda Songea. Halafu, hakuna basi la Mwanza-Iringa/Njombe?
 
Kufika njombe ni siku mbili chukua gari ya kutoka mwanza adi mbeya ambayo itakufikisha mida ya SAA moja hivi usiku ukipanda asubuh SAA kumi na mbili utashukia makambako ambapo utapanda gari nyingne ya kukufikisha njombe na pia andaa makoti mablanket ya kutosha sababu kuna bardi Kali San na watu wa huko ni wakarmu tu karbu nyanda za juu mkuu
Aisee siku mbili!! harafu kumbe mpaka ufike mbeya!!! Ahsante mkuu pamoja sana!
 
Msaada wako mkuu tafadhali sijawahi kufika huko naomba kama unapajua zaidi!
Mkuu, mkoa wa Njombe una Wilaya nyingi zikiwemo Njombe, Ludewa na Makete. Unakwenda ipi? Nakushauri kwanza upate usafiri wa kukufikisha Iringa. Halafu, kuanzia hapo, unaweza kufika katika Wilaya husika ya mkoa wa Njombe. Naamini, yapo mabasi ya Mwanza-Iringa/Njombe.
 
Ahsante mkuu naenda Njombe mjini, nimeshtuka kidogo nilipoona mwanaJf mwenzetu anasema mpaka nifike mbeya!!
 
Kidogo kupunguza kupanda basi nyingi since unamizigo panda za kwenda iringa then utapata za mojamoja mpaka njombe though ni safar ya siku mbili pia..Ila nenda na makoti baridi ipo vzur kipindi hiki
 
Sawa, kama ni Njombe Mjini, tafuta basi la Mwanza-Iringa/Njombe. Hapo utakuwa umemaliza. Ukifika Iringa, panda basi la Njombe au yale yanayokwenda Songea na ushuke Njombe. kama wanavyodokeza wadau, Njombe kuna baridi sana. Jiandae. Jambo la msingi ni kuheshimu wenyeji na kuyasoma mazingira kabla ya kufanya lolote.Kila la kheri!
 
Na uzur ni kwamba utanikuta na heka zang kadhaa za viazi nakaribia kuvuna,bar maarufu ni Giraf,ila barid barid barid barid,,ukija kabla ya alhamis utanikuta nitakupa muongozo vzr kijana,karib ila ukimwi kama alietangulia kusema upo sana kwa mujib wa repot ya taifa
 
Ahsante kiongozi!
 
sawa mkuu nimekuelewa! kama una chochote cha kuniongezea usisite kufanya hivo!
 
Ohh! vizuri kiongozi vipi mjini upatikanaji wa maji upoje huko!
 
sawa mkuu nimekuelewa! kama una chochote cha kuniongezea usisite kufanya hivo!
Ukinisoma hapo, utaona kuwa nimemaliza kila jambo unaloweza kulifikiria. Kiujumla, uende ukabehave na ujue kuwa Maisha katika mkoa huo, kama ilivyo kwa Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa ni nafuu kama utajipanga vyema.
 
Salaam wanaJf,

Mwishoni mwa wiki hii nina safari ya kwenda mkoa wa Njombe nitakuwa huko kwa mda mrefu kidogo, kwa hiyo naenda kuanza makazi mapya natokea mwanza, sijawahi kufika huko.

Natamani/napenda kujua usafiri wa kutoka mwanza hadi huko kwanza ni gari ipi inayofika huko na ubora wa gari lenyewe, barabara ikoje kwa sababu nitakuwa na mizigo ambayo ikipata barabara mbaya inaweza isifike ikiwa salama, Ni masaa mangapi kutoka mwanza hadi huko,

Hali ya hewa ikoje, watu wake je! vipi kuhusu upatikanaji wa maji, maisha yakoje huko? upatikanaji wa nyumba za kuishi gharama zikoje?

Msaada wenu wakuu naamini humu kuna wenyeji wazaliwa na wakazi wa huko!
Kwa basi zuri ni Katagi
 
Back
Top Bottom