Naomba kujua kihusu mikopo.

Messenger RNA

JF-Expert Member
Jul 24, 2022
1,102
3,022
Iko hivi kuna rafiki yangu alikopa kwenye hizi microfinance kwa makubaliano ya kulipa baada ya mwaka mmoja na aliweka nyumba kama dhamana ,lakini mambo yalimwendea ndivyo sivyo pesa ikavurugika,sasa jamaa baada ya kuona hivyo akakimbia bila hata kunishirikisha.
Msaada wangu kujua kisheria:- 1.tunaweza kushawishi kuongeza muda wa kulipa mkopo?
2.wanaweza piga bei kiwanja hata kama mwenye nacho hayupo?.
-Naomba msaada nataka nisaidiane na mkewe kuokoa nyumba watoto wasije dhalilika.
 
Pole mkuu, dawa ya deni kulipa usije ukadhalilika na familia yako

Funzo: usikope kwenye hizi microfinance wana majanga sana
 
Kwani mkuu unahisi kwanini nyumba iliwekwa dhamana?

Unaelewa uhusiano uliopo kati ya deni, mwaka mmoja wa kulipa na nyumba? Kama ukiuelewa huu uhusiano wala usingepaniki mkuu, ungeanza kuhamisha fanicha na kutafuta pa kupeleka familia.

Achaneni na ujanja eti jamaa kakimbia unataka kuokoa watoto wasidhalilike. Hakuna utetezi kama huo. Nadhani kila kitu kilikuwa straight kabisa tangu mwanzo nini kitatokea kama mwaka utaisha na hela haitalipwa.

Na uzuri mikopo huwa inatolewa baada ya consent ya mke au mume. So mke anajua kila kinachoendelea
 
Iko hivi kuna rafiki yangu alikopa kwenye hizi microfinance kwa makubaliano ya kulipa baada ya mwaka mmoja na aliweka nyumba kama dhamana ,lakini mambo yalimwendea ndivyo sivyo pesa ikavurugika,sasa jamaa baada ya kuona hivyo akakimbia bila hata kunishirikisha.
Msaada wangu kujua kisheria:- 1.tunaweza kushawishi kuongeza muda wa kulipa mkopo?
2.wanaweza piga bei kiwanja hata kama mwenye nacho hayupo?.
-Naomba msaada nataka nisaidiane na mkewe kuokoa nyumba watoto wasije dhalilika.
Kimsingi lengo la benki sio kuuza nyumba bali ni kulipwa pesa zao hivyo basi mnàweza kumwona branch manager mkamwambia mnaweza kuongezewa muda
 
Back
Top Bottom