Naomba kujua gharama za kuanzisha kituo cha TV

MrIsidori

Senior Member
Apr 3, 2014
191
83
Naomba kama kuna anayejua gharama ya kuanzisha kituo cha TV anijulishe taratibu zote gharama kwa ujumla.
 
Kwanza unatakiwa kujua scale ya kituo unachotaka kuanzisha kwa maana ya unataka kituo cha ukubwa gani na ungependa zaidi kujihusisha na aina gani ya matangazo!

Hatua ya pili mwone mpembuzi yakinifu wa miradi whom atakushauri kulingana na kiwango chako cha hela unachotaka kuwekeza kwenye mradi tajwa.

Tatu utaonana na msanifu wa Majengo/Architect akubunie Jengo ama kukufanyia ubunifu wa ndani ikiwa jengo si lako/ikiwa umepata pango ili lilweze kuendana na vifaa vya studio na kuweza kumonitor sauti ya ndani kutotoka nje na nje kutoingia ndani!

Baada ya zoezi hilo kukamilika unaenda Brella kuandikisha mradi kisha unapitia mamlaka ya mawasiliano/TCRA ili upewe leseni ya kurusha matangazo na masafa ya kurushia matangazo!

Baada ya hapo pitia DSJ chukua vijana wawili watatu wanaosomea utangazaji kisha tafuta mkongwe mmoja mcharuko changanya na damu changa kitu kideoni!
 
Naomba kama kuna anayejua gharama ya kuanzisha kituo cha TV anijulishe taratibu na gharama zote kwa ujumla mpaka iwe hewani.
 
Unataka alafu iweje....??? haya ngoja nikwambie ni milioni moja na nusu...taslimu
 
Kituo kama Azam Tv, Gharama zake ni kama Billion hamsini na kitu. Kwa mujibu wa Taarifa ya habari ya ITV.
 
Cha kwanzani kuwa na WAZO na maoni ya kuanzisha kitu hiki. Hapa unaonekana umepatia. Pili unatakiwa kuwa na pesa kiasi fulani kwa ajili ya establishment. Nafasi yakuweka kituo: nafasi, jengo,n.k. Unahitaji kuwa na utaalamu wewemwenyewe au waliosomea. Unataka kuanza na vifaa vichache: Video camera, computer kwa ajili ya editing na kutengeneza vipindi, pamoja na TV transmitter. Lakini unahitji kuwa na masafaa ambapo hapo unahitaji kuwafikia waratibu mawasiliano kitaifa: ambao ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Kusema kweli, hatua ya kwanza baada ya kupata wazo, nenda Mawasiliano Towers karibu na Mlimiani City pale Sinza. Uliia ofisi za wanaohusika na TV broadcastaing watakupa msaada wowote unaohitaji tena bila gharama yeyote!!
 
Back
Top Bottom