Naomba kujua elimu hii kuhusu kulipa kodi za TRA

mfuga kuku

JF-Expert Member
Jul 14, 2014
750
544
Habari za asbh Wana bodi wenzangu!

Naomba nijulishwe kwa mwenye uzoefu juu ya Jambo hili.

Nina miliki kasteshenari huku mikoani, Mwaka Jana wakati nakaanzusha nikalazimika kutafuta leseni ya biashara, huko nikalazimika lazima nianze kwanza TRA ili kupata Tax clearance, nikafanyiwa makadirio ya kulipa Tsh 62,500/= kwa kila robo Mwaka, yenye jumla ya Tsh 250,000/= kwa Mwaka, nikajipiga piga na kwa kuwa biashara ndio nilikuwa naanza lkn nikafanikiwa kulipa pesa yote ktk robo zote nne.

Sasa Mwaka huu nikarudi tena TRA kwa ajili ya kukadiriwa Tena, nukakutana na ongezeko la kutakiwa kulipa Tsh 400,000/= kwa Mwaka ambapo kwa kila robo Mwaka natakiwa kulipa 100,000/= kuwa sina Elimu hii naomba kwa yeyote mwenye kujua, hiyo fedha ni halali yangu au nachomekewa tu? Maana Wala hatujazungumza afisa ananambia Mwaka huu unatakiwa kulipa 400,000/= kwa Mwaka na kila robo utalipa 100,000/=
 
Unaweka kumbumbuka za biashara yako? Amezipitia na kukuonyesha basis ya computation ya assessment?
 
Hajapitia kumbukumbu yoyote ya biashara yangu! Amenitamkia tu mdomoni, biashara yangu hata EFD bado sijafanikiwa kuwa nayo nahisi labda ningekuwa nayo ingekuwa rahisi kwake kujua mauzo yangu.
 
Sasa kakukadiria kutumia kigezo gani??
 
Sasa kakukadiria kutumia kigezo gani??
Afisa wa TRA anadai kila Mwaka lazima Kodi iwe inapanda na huwa inapanda mapema wakati wa bajet za serikali hivyo Sina nafasi ya kuomba nipunguziwe kodi, isipokuwa Kuna nafasi ya kufunga biashara endapo Kama nahitaji kufunga biashara amenitaka niandike barua
 
Kwa kweli hata Mimi nimeshangaa! Ndio maana nikaona nililete huku mnipe akili mpya, kwa kuwa nami Sina Elimu ya Kodi nikajua ni sawa tu!
Mambo bana ya hao wakadiria kodi wakati mwingine ni jinsi mtu anavyojisikia tu!!kama huna records ya mauzo!!ila inatakiwa akuulize mauzo yako ya siku, yakoje ndio akukadirie kodi, hiyo karatasi aliyokukadiria tayari umeshaichukua?kama meshaichukua hapo tena ndio imetoka tena hakuna jinsi!!
 
Afisa wa TRA anadai kila Mwaka lazima Kodi iwe inapanda na huwa inapanda mapema wakati wa bajet za serikali hivyo Sina nafasi ya kuomba nipunguziwe kodi, isipokuwa Kuna nafasi ya kufunga biashara endapo Kama nahitaji kufunga biashara amenitaka niandike barua
Sio kweli kuwa kila mwaka kodi lazima ipande, kodi inapanda kutokana na biashara yako kukua!!mauzo yanavyozidi kuongezeka na kodi inatakiwa kuongezeka pia.
 
Afisa wa TRA anadai kila Mwaka lazima Kodi iwe inapanda na huwa inapanda mapema wakati wa bajet za serikali hivyo Sina nafasi ya kuomba nipunguziwe kodi, isipokuwa Kuna nafasi ya kufunga biashara endapo Kama nahitaji kufunga biashara amenitaka niandike barua
hii elimu ya kulipa kodi inahitajika sana hasahasa mtaani vinginevyo wakwepa kodi hawawezi kupungua,nijuavyo me watu hufungua biashara na kufunga kila baada ya kufunga hesabu zao TRA nadhani hii ndosababu
 
Elimu ya kulipa Kodi kwa kweli bado Ina hitajika hasa kwa tulio wengi! Tunatamani Sana kuchangia pato la Taifa letu lkn TRA MNATUKATISHA TAMAA, MMEJAWA NA TAMAA ZENYE KUICHAFUA SERIKALI KWA RAIA WAO.
 
Bottom line is, keep rekord of your business, hii ndio itakuokoa kwenye kupinga makadirio. Vinginevyo utaishia kuja kulalamika jf na kupewa ushauri wa ki-layman
 
Habari za asbh Wana bodi wenzangu!

Naomba nijulishwe kwa mwenye uzoefu juu ya Jambo hili.

Nina miliki kasteshenari huku mikoani, Mwaka Jana wakati nakaanzusha nikalazimika kutafuta leseni ya biashara, huko nikalazimika lazima nianze kwanza TRA ili kupata Tax clearance, nikafanyiwa makadirio ya kulipa Tsh 62,500/= kwa kila robo Mwaka, yenye jumla ya Tsh 250,000/= kwa Mwaka, nikajipiga piga na kwa kuwa biashara ndio nilikuwa naanza lkn nikafanikiwa kulipa pesa yote ktk robo zote nne.

Sasa Mwaka huu nikarudi tena TRA kwa ajili ya kukadiriwa Tena, nukakutana na ongezeko la kutakiwa kulipa Tsh 400,000/= kwa Mwaka ambapo kwa kila robo Mwaka natakiwa kulipa 100,000/= kuwa sina Elimu hii naomba kwa yeyote mwenye kujua, hiyo fedha ni halali yangu au nachomekewa tu? Maana Wala hatujazungumza afisa ananambia Mwaka huu unatakiwa kulipa 400,000/= kwa Mwaka na kila robo utalipa 100,000/=
Mkuu,Kwanza Fanya makadirio yako mwenyewe online,lipa mwenyewe online itakuondolea hizo STRESS za kuambiwa tu LIPA hii.Pili fanya mpango uwe na EFD kama unahitaji EFD kwa bei nafuu nicheck PM.Kama unahitaji mwongozo jinsi ya KUJIKADIRIA mwenyewe pia nicheck PM.

Mwisho unayo haki ya kupinga makadirio kama unaona yako juu sana kuliko uhalisia wa biashara yako.Zingatia KODI ya PANGO unapofanyia biashara nayo inaweza kuwa ni kubwa.All in All unahitajika kunicheck PM.

LIPA KODI KWA MAENDELEO YA NCHI
 
Nenda tena kwa afisa wa TRA hasa kamuone meneja. Mwambie biashara yangu ndio kwanza unaanza,bado sijatengeneza hata wateja,mtaji nao ninao kidogo. Hii kadirio ni kubwa kwangu. Uwezo wa ofisi yangu ni laki 250,kama nilivyokadiriwa mwaka jana wakati naanza. Atakupunguzia tu,ila Ndio njia yao ya kukupiga. Lazima mpatie hata elfu 50

Wenyewe hesabu yao ni mbovu tu. Wana-assume biashara inakuwa kila siku. Hawapigi kwenye kurudi nyuma au hasara.
 
Sheria ipo wazi kabisa kwa mfanyabiashara siweza kitunza kumbukumbu basi kima cha chini kwa mara ya pili ni 100,000 kama ulivyoshauriwa kuwa na daftari andika mauzo yako ya kila siku. Weka kumbukumbu za matumizi. Ili utoke kwenye kundi la wasiotunza kumbukumbu na utakadiriwa kulingana na mapato na matumizi yako.
 
Nenda tena kwa afisa wa TRA hasa kamuone meneja. Mwambie biashara yangu ndio kwanza unaanza,bado sijatengeneza hata wateja,mtaji nao ninao kidogo. Hii kadirio ni kubwa kwangu. Uwezo wa ofisi yangu ni laki 250,kama nilivyokadiriwa mwaka jana wakati naanza. Atakupunguzia tu,ila Ndio njia yao ya kukupiga. Lazima mpatie hata elfu 50

Wenyewe hesabu yao ni mbovu tu. Wana-assume biashara inakuwa kila siku. Hawapigi kwenye kurudi nyuma au hasara.

Huwezi kujitetea kwa kupiga porojo, dokument/ rekodi za biashara yako ndio zinaongea. Ndio zitakusaidia unapojitetea, Müache kufanya biashara kama malumpeni.
 
Mkuu,Kwanza Fanya makadirio yako mwenyewe online,lipa mwenyewe online itakuondolea hizo STRESS za kuambiwa tu LIPA hii.Pili fanya mpango uwe na EFD kama unahitaji EFD kwa bei nafuu nicheck PM.Kama unahitaji mwongozo jinsi ya KUJIKADIRIA mwenyewe pia nicheck PM.

Mwisho unayo haki ya kupinga makadirio kama unaona yako juu sana kuliko uhalisia wa biashara yako.Zingatia KODI ya PANGO unapofanyia biashara nayo inaweza kuwa ni kubwa.All in All unahitajika kunicheck PM.

LIPA KODI KWA MAENDELEO YA NCHI
Hapo kufanya makadirio online ni kwa ambao wanaanda mahesabu ya mwisho wa mwaka tuu. Sasa kikubwa hapo ni huyo ofisa angeweka increment ya kodi lakini sio kubwa kiasi hicho. Na kuhusu EFD mashine usimpotoshe huyu jamaa kwa maana bado hujajua anauza kwa kiasi gani.Sio kila mtu anatakiwa kununua mashine ya EFD labda kama mauzo yamefikia 11M kwa mwaka ndo atanunua mashine. Kikubwa amuonyeshe rekodi ya mauzo anayoweka kwenye daftari hapo ndo itakua pona yake.
 
Huwezi kujitetea kwa kupiga porojo, dokument/ rekodi za biashara yako ndio zinaongea. Ndio zitakusaidia unapojitetea, Müache kufanya biashara kama malumpeni.
Wewe ndio unaropoka hujui kitu niko kwenye biashara mwaka wa 11 kwenda kujitetea ni kitu cha kawaida. Document record gani unazolazimisha? Biashara ameanza mwaka jana,hana mashine ya risit inayotunza record.

Usimsikilize huyu kenge. Wewe nenda kwa meneja moja kwa moja
 
Back
Top Bottom