Naomba kufahamu zilipo ofisi hizi

Naomba kufahamu zilipo ofisi hizi

Mwakabizzle

Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
29
Reaction score
2
Tusaidiane wakuu,
Naomba kujuzwa ilipo ofisi za Unique Consultancy Service na ninachojua ni kuwa wapo kwenye jengo la New Red Cross Building ila tatizo ni kwamba sijui maeneo lilipo hilo jengo na linatazamana na jengo gani au ofisi gani itakayonisaidia kutambua kwa haraka.....

Na pia naomba msaada wa kufahamu zilipo ofisi za Proactive Employment Solutions (PES) kuna jamaa mmoja ameniambia kuwa wapo mbezi beach lakini sijui kituo cha kushukia kama natokea mwenge na jengo ambalo ofisi hii inapatikana linaitwaje au lipo jirani na jengo gani au kampuni gani kama alama ya kuniwezesha kufika hapo.

Naomba msaada wakuu mimi ni mgeni yaani si mwenyeji sana hapa Dar es salaam kwa hiyo nahitaji mwongozo wenu kwa ofisi tajwa hapo juu.

Shukrani na heshima kwenu wakuu.
 
Tusaidiane wakuu,
naomba kujuzwa ilipo ofisi za Unique Consultancy Service na ninachojua ni kuwa wapo kwenye jengo la New Red Cross Building ila tatizo ni kwamba sijui maeneo lilipo hilo jengo na linatazamana na jengo gani au ofisi gani itakayonisaidia kutambua kwa haraka.....

Na pia naomba msaada wa kufahamu zilipo ofisi za Proactive Employment Solutions (PES) kuna jamaa mmoja ameniambia kuwa wapo mbezi beach lakini sijui kituo cha kushukia kama natokea mwenge na jengo ambalo ofisi hii inapatikana linaitwaje au lipo jirani na jengo gani au kampuni gani kama alama ya kuniwezesha kufika hapo.

naomba msaada wakuu mimi na mgeni yaani si mwenyeji sana hapa Dar es salaam kwa hiyo nahitaji mwongozo wenu kwa ofisi tajwa hapo juu.
Shukrani na heshima kwenu wakuu.

Naomba nijibu kipengele cha pili, Proactive Employment Solutions (PES) wapo Mbezi beach. Shukia kituo cha Tangibovu then panda bajaji ama bodaboda halafu waambie wakupeleke rainbow kwa mguu kuna kaumbali kiaina kutokea Tangibovu
 
Wewe ni last born? Una Elimu gani? Je ni me au ke? Hizo ofisi unazozitafuta hazina tovuti? Na kama zinazo , je ni kweli umeshindwa kujua zilipo kupitia tovuti zao?

Aaah sio kweli bhana!
 
Tukipata namba zao ndo ingekuwa bora zaidi sababu kwa njia tovuti inakuwa ngumu wakuu..
 
Back
Top Bottom