Kwenye taa ninakubaliana na wewe asilimia 200. Kuna jamaa yangu anaishi kwenye flat fulani hivi lina mambo mengi sana yanaendelea pale, jamaa wawili wanaoishi kwenye flat hilo, walifanya mpango wakaleta mafundi wa NJE wa umeme, wakaja wakadisconnect taa za kwenye ngazi, halafu wakadai kuwa nyaya zimeungua. Kwa hiyo kwenye ngazi huwa kuna giza totoro usiku. Maghorofa ni ya umma, na mafundi wahusika wa wa Tasisi husika wa umeme wapo lakini wao walienda wakachukua mafundi kutoka mtaani. Zaidi ni kuwa kuna maghorofa mengine matatu jirani yanayofanana na ghorofa hilo, yenyewe taa zake ziko sawa, hayana pilika pilika za usiku.
Cha kushangaza zaidi pia ni kuwa kuna jamaa yao mmoja ghorofa hilo hilo, amekatiwa maji nyumba nzima tangu Novemba 2018, karibia miaka miwili sasa, mpaka leo hana maji wakati kila mwezi huwa anakatwa elfu 25 kwa ajili ya maji. Mpango ulisukwa mwanzoni ikaonekna kuwa ghrorfa zima halina maji, halafu baadaye yakarudi, yeye hana mpaka leo.
Wameweka mpira wa maji wa kupandisha juu,kwenye bomba la nje linalotoa maji, mpira ambao yeye akitaka kuutumia, lazima afanye Ibada kwanza, vingnevyo akichota tu hayo maji kwa kutumia mpira huo, usiku hawezi kulala, au gari lake kesho asubuhi haliwezi kupiga stata kwenda kazini.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 200 kwenye issue ta taa!