Naomba kufahamu kuhusu Toyota Altezza

Mzembe flani

Senior Member
Jul 1, 2019
190
208
Habari wakuu,

Nimekuwa nikipitia nyuzi nyingi kuhusu magari tofauti lakini sijabahatika kukutana na uzi ukijadili Toyota Altezza na Subaru Legacy ni gari ambazo natamani kununua.

Naomba kufahamishwa pros and cons zake, binafsi sina uzoefu au ujuzi wa magari, hivyo nategemea kupata maoni yenu wataalamu.

Asanteni.
 
Altezza Toyota
Legacy Subaru
Wote ni Wajapani..ila wana philosophy tofauti..!

Toyota Altezza imekuja na options 2 za engine 4 cylinders 3S na 6 cylinders 1G..3S kwenye makaratasi ina nguvu zaidi ya 1G..ila 1G ni imara kweli kweli..!
Kama unachukua 3S jitahidi iwe manual..!
 
Alteeza ni Habari nyingine, iyo ni sport-car old fasion - tafuta ile ya engine ya YAMAHA G-20 Hutojutia Gari inakimbia mnoo. Ila jipange kwenye wese town trip daily Cost si chin ya mafuta ya Elf 30,000/=.
 
Altezza Toyota
Legacy Subaru
Wote ni Wajapani..ila wana philosophy tofauti..!

Toyota Altezza imekuja na options 2 za engine 4 cylinders 3S na 6 cylinders 1G..3S kwenye makaratasi ina nguvu zaidi ya 1G..ila 1G ni imara kweli kweli..!
Kama unachukua 3S jitahidi iwe manual..!
Hapa umemshauri kimbio zaidi ila kwa maintainance nafuu ni heri achukue altezza yenye injini ya 1gFE, kwasababu spea zake zinapatikana kwa wingi kwakuwa injini hiyo ipo kwenye magari mengi tofauti mf;gx 100 zote (cresta, mark ii & chaser) mark ii grande gx 110, verossa na kadhalika ilhali injini ya 3sGE ipo kwenye toyota altezza tuu hivyo ni injini adimu na vipuli vyake ni ghali. Kwa mfano wiki iliyopita nimeulizia coil ya plug ya altezza 3sGE shaurimoyo ikawa inacheza kwenye laki ilhali coil za 1g ni elfu 40. Injini ya 3sGE used kutoka Dubai ni milioni 3, injini ya 1g used kutoka Dubai complete sina uhakika ni bei gani ila mswaki nasikia mpaka laki 5 unapata. Ila kwa mwendo 3sGE inatembea kuliko 1gfe na akipata yenye manual transmission basi hata crown za 4gr-fse atakuwa anazipa dozi.
 
Alteeza ni Habari nyingine, iyo ni sport-car old fasion - tafuta ile ya engine ya YAMAHA G-20 Hutojutia Gari inakimbia mnoo. Ila jipange kwenye wese town trip daily Cost si chin ya mafuta ya Elf 30,000/=.
mimi sipo mjini ya dar mzee, niko mjini iringa mizunguko sio mingi, pia route za mkoa kwa mkoa ni moja ndani ya miezi miwili na haizidi 3. ndani ya miezi miwili.
 
Kama huna uzoefu wa magari achana na subaru na hiyo altezza yenye 3s pia achana nayo. Chagua gari ambayo ni common na imezoeleka hasa toyota itakusaidia kwenye matengenezo, spea, na kuvumilia kutokuwa kwako na ujuzi maana gari yako ya kwanza ndiyo itakayokufunza mambo mengi kuhusu magari haswa pale unapokosea baadhi ya vitu hivyo ni vyema ukawa na gari ambayo inaweza kuvumilia baadhi ya makosa utakayofanya ya upungufu wa matunzo mf: kuitembelea huku ina upungufu wa oil, upungufu wa coolant/maji nakadhalika. Kwa mimi nakushauri utafute gari yenye injini ya 1gfe (nimeziorodhesha hapo juu) kwa uzoefu wangu naona ni injini vumilivu na sio ghali kuitunza. Japokuwa gari sio injini peke yake ila injini ni moja kati ya main components za gari.
 
naomba uidadavue niifaham vyema
Kuna subaru zenye turbo na zisizo na turbo. Gari zenye turbo zina tabia tofauti kidogo na gari zisizo na turbo ni vyema ukafafanua legacy unayovutiwa nayo ni ipi kati ya hizo. Pia design ya injini ya subaru mpangilio wake wa piston ni tofauti (boxer) design hii inazisumbua hizi gari kwenye kutunza oil baadhi ya vifaa kwenye injini zake vikianza kuchoka haswa seals za oil hivyo ni makini kuwa unaichunguza kiwango cha oil mara kwa mara. Kuna baadhi ya matoleo ya subaru i.e wrx na wrx sti (imprezza zenye turbo) zina ugonjwa wa kuunguza cylinder head gasket japokuwa mara nyingi husababishwa na uendeshaji wa mtu japokuwa sina uhakika kuhusiana na tatizo hilo kwa subaru ambazo hazina turbo. Huo ndo ufahamu kidogo nilioung'amua kwenye subaru. Wajuzi wataongezea zaidi.
 
Back
Top Bottom