Naomba kufahamu kuhusu hawa samaki

Naomba kufahamu kuhusu hawa samaki

solanum

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
203
Reaction score
99
Habari zenu wakuu,

Ni hivi kuna samaki wanaitwa NGURUKA nahitaji kujua hawa samaki ni aina gani na wanapatikana ziwa, mto au bwawa gani hapa Tanzania.
 
nguruka wanapatikana nguruka ipo wilaya ya Uvinza,!wanapatikana kwenye kiziwa/bwawa linaitwa Sagara kama sijakosea ila kwa hapa Tz utawapata kwa wingi Mkoani Morogoro
 
Mkuu unanikumbusha chuo wakat nasoma pale sua
 
Umenikumbusha mbali sana.
Nilipokuwa Moro wakati fulani (nilikuwa katoto) nilitumwa hao nguruka.
Kwa uroho wangu wa samaki na kwa sifa nilizozisikia kuhusu utamu wa nguruka nikaona isiwe case...ngoja nidokoe kabla sijawafikisha home.
Ladha niliyokutana nayo hadi leo nikiwaona najisikia vibaya.
Ilikuwa kama magadi hiviiiiii...

Kufika home nikamueleza mamdogo ukweli kuwa hawa samaki mbona sio watamu kama mnavyowasifu?
Alicheka sana...akaniambia sikupaswa kuwala kabla hawajachomwa.
Daaaah hata alipowachoma na kunipa nilikataa kabisa.
 
pole
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom