Naomba kufahamu huu ni ugonjwa gani

GANG MO

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
2,087
2,194
Habari ya majukumu wadau wa kilimo na ufugaji. Nimefuga kuku wa kienyeji. Wiki iliyopita niliona kuna kuku amepoa sana. Sasa kadiri siku zinavokwenda. Huyu kuku anavimba eneo la jicho mpaka haoni. Naombeni mnijuze aina ya ugonjwa na matibabu yake. Natanguliza shukrani
20181204_184220.jpg
 
Mbona Hiyo ni ndui uliwapa chanjo ya ndui
Kama sikosei wanasema ni corayza
Na kuna dawa ya kuwawekea kwenye maji wanywe
Pia unatakiwa umsafishe macho kwa pamba ambapo utatakiwa kumtoa huo uchafu huko machoni ambao unakuwa utando mweupe ukisha msafisha ndipo unamwekea hiyo dawa kwenye macho
 
Maelezo kidogo mdau. Gumboro ni ugonjwa wa unaosababishwa na nini? Na vipi kuhusu matibabu ?
Ni ugonjwa unaoambatana na ndui na kuna chanjo yao kuna ilw ya matone kwenye macho na ile ya sindano kwenye mabawa majina yamenitoka au unanunua ile inaitwa E.s.b 3. (I esi bii three)
 
inaitwa Infectious coryza ni ugonjwa hatari wa bacteria ambao unaathiri mfumo wa upumuaji na huwa unaonekana kwa kuvimba macho na eneo chini ya jicho, kuku kutoa makamasi na kupiga chafya ugonjwa huu husababisha hasara kubwa.
cha kufanya
chukua wembe pasua huo uvimbe utatoa kitu cheupe kama gololi. weka dawa ya kidonda au paka ute wa jani la aloevera
safisha banda tumia dis infectant ya v-rid 20ml changanya na maji lita kumi na tano wape kuku vitamini kwenye maji,maana pia kupungua kwa vitamin A husababisha washikwe ugonjwa huo kirahisi. walishe majani kwa wingi na chakula kamili kutokana na umri wao. unaweza kutibiwa kwa kutumia antibiotic na dawa zenye salfa. uaweza kupata ushauri zaidi duka la dawa za mifugo

wafugaji wengi wanashindwa kutofautisha kati ya ugonjwa huu wa coryza na fowl pox (ndui)

fowl pox (ndui) wanakuwa na vidoti na madonda madonda mwili mzima mpaka hata baadhi ya sehemu za miguu na ukifunua mwanyoya na mabawa utaviona
coryza ni kama inavyoonekana kwenye picha

https://web.facebook.com/makurainvestment/
 
Attachments

  • pox.PNG
    pox.PNG
    148 KB · Views: 123
  • coryza.PNG
    coryza.PNG
    220.1 KB · Views: 108

Thanks kwa DARASA! Mimi wangu wamepata chanjo hadi ndui lakini wananyongonyea na kushuka mabawa halafu wanakufa, Yawezekana ni Ugonjwa gani hasa
 
kama chanjo umewapa jaribu kuangalia kinyesi chao kina rangi gani. kama kina rangi ya ugoro au rangi ya kahawia au pengine wanaharisha damu. pengine ikawa cocissidiosis au typhoid. kunyongonyea na kushuka mabawa ni dalili ya magonjwa mengi. link ya ndondo ambazo zitakusaidia. unaweza kuchkua mmoja wapo ukapeleka kwenye duka la dawa kama pana daktari anaweza kumpasua na kuangalia.

pata kijitabu hapo kitakusaidia

http://ufugaji.co.tz/wp-content/uploads/2015/09/MAGONJWA-MAKUU-YA-KUKU-TIBA-NA-KINGA.pdf
 
Ndugu! Mimi pia vifaranga vyangu vya kuku wa kienyeji vimeshambuliwa na macho yameziba kabisa. Ni hatari huu ugonjwa.
 
Magonjwa ya kuku yanaumiza sana wafugaji wengi, mie pia nimepitia sana hizo changamoto pamoja na kutumia gharama kwenye madawa mara nyingine hazisaidii inakua kama bahati nasibu hasa pale ugonjwa unapokua ushawapata...
Kwa sasa nimeacha kabisa tumia madawa ya kununua, ni mwendo wa alovera, oregano na vitunguu swaumu tokea wanapoanguliwa na nashukuru tokea nimeanza hizi tiba mbadala huu ni mwaka na miezi 2 kuku hawajawahi kufa wala kushambuliwa na ugonjwa hatarishi...
 
inaitwa Infectious coryza ni ugonjwa hatari wa bacteria ambao unaathiri mfumo wa upumuaji na huwa unaonekana kwa kuvimba macho na eneo chini ya jicho, kuku kutoa makamasi na kupiga chafya ugonjwa huu husababisha hasara kubwa.
cha kufanya
chukua wembe pasua huo uvimbe utatoa kitu cheupe kama gololi. weka dawa ya kidonda au paka ute wa jani la aloevera
safisha banda tumia dis infectant ya v-rid 20ml changanya na maji lita kumi na tano wape kuku vitamini kwenye maji,maana pia kupungua kwa vitamin A husababisha washikwe ugonjwa huo kirahisi. walishe majani kwa wingi na chakula kamili kutokana na umri wao. unaweza kutibiwa kwa kutumia antibiotic na dawa zenye salfa. uaweza kupata ushauri zaidi duka la dawa za mifugo

wafugaji wengi wanashindwa kutofautisha kati ya ugonjwa huu wa coryza na fowl pox (ndui)

fowl pox (ndui) wanakuwa na vidoti na madonda madonda mwili mzima mpaka hata baadhi ya sehemu za miguu na ukifunua mwanyoya na mabawa utaviona
coryza ni kama inavyoonekana kwenye picha

https://web.facebook.com/makurainvestment/
Ahsante sana kwa ushauri mzuri mdau
Ubarikiwe sana
 
Kama wana ndui tafuta dawa ya binadam inatwa pen V weka kidonge kimoja kwenye maji siku 7 biashara kwisha
 
Dudupori, umeweka vitu vitatu hapo, kwenye maelezo yako arovera, vitunguu swaumu na kingine hicho in nini?
 
Back
Top Bottom