JE NINA TATIZO GANI LA KIAFYA.

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
7,621
16,700
Habari wakuu.

Nimeamka nije hapa Jamii Forum niweze kupata Ushauri WENU ndugu zangu.

Ninasumbuliwa na Ugonjwa kwa Miezi Mitatu sasa.

Historia Fupi ya Ugonjwa.

Nilikuwa nasumbuliwa na kikohozi kikavu kwa week Tatu kuanzia Tarehe Tano 5 Desember 2022 Hadi 23 Desember 2022.
Ndipo nilipona Baada ya kutumia helbal medicine

Sijawahi kuugua kikohozi Maishani MWANGU.

Nikalazimika kutumia Tangawizi kwa wiki Nzima bila nafuu yoyote.
Nikatafuta mchanganyiko wa kitunguu + Limao + Majani ya Limao + Tangawizi.
Nikanywa kwa wiki Tatu.
Bila nafuu yoyote.

Ghafla tarehe 20 Desember nikajihisi Ugonjwa Homa Kali sana.
Baada ya siku Mbili vidonda vya tumbo vililipuka yaani tarehe 22.

Niliwahi huugua vidonda na kupona miaka Saba iliyopita. Lakini vilirudi Mwaka 2022.

Nimejaribu kutumia Kila aina ya Dawa bila mafaniko.
1. Nimetumia Dawa za muhimbili.
2. Nimetumia Dawa za Tiba mbadala Muhimbili.
3. Nimetumia Kila aina ya Dawa hata kutoka Congo Malawi nk.
4. Nimetumia Dawa karibia 20 lakini tatizo Bado linanisumbua Mno.

1. Ninapata maumivu makali sana Pale ninaponyanyua kitu chenye zaidi ya kilo Kumi.

2. Nikijinyoosha usiku ninapatwa maumivu makali sana.

3. Ninashindwa na kazi ndogo sana kufagia chumbá, kufua nk.

Nimesitisha MATUMIZI ya vyakula kama Tangawizi, pilau, Dagaa,
Maharage, Juice, soda nk.

NIMEKUJA KWENU NDUGU ZANGU MPATE KUNISAIDIA.
NAOMBENI MSAADA WENU.
NATANGULIZA SHUKRANI.
 
Umebadili mazingira ya kuishi au uko eneo lako la siku zote? .

Mazingira ya kAzi je? Uko nayo comfortable?

Uko nayo comfortable?

Mahusiano yako yapo normal? (Mke, famili, jamii n.k)
 
Pole mkuu lkn kama shida ni vidonda vya tumbo tumia unga wa manjano ule mpya [ambao haujakaa sku nyingi unachukua maji ya vuguvugu kikombe cha chai unawekà kijko 1 cha chai cha huo unga na asal mbchi kijiko 1 kikubwa unakoroga unakunywa kutwa mara 3 kwa wik 3...mwezi tu
 
Nilituma sana manjana mkuu.

Nimetumia hadi binzali week mbili Lakini wapi.
 
Umebadili mazingira ya kuishi au uko eneo lako la siku zote? .

Mazingira ya kAzi je? Uko nayo comfortable?

Uko nayo comfortable?

Mahusiano yako yapo normal? (Mke, famili, jamii n.k)

Kila kitu kipi sawa mkuu.

Sijabadiri chochote.

Zaidi ya safari za Dodoma Dar.
Dar Dodoma.
 
Pole sana, kuna sehem niliskia sa sijui ulikuw ni utani au la

Ukiamka Asubuhi piga maswaki bila dawa, then meza yale mate kwa muda wa wiki mbili utapata majibu.. Vidonda vitaisha.

Weka nia na imani.. Try.
 
Mkuu hata frolide siitumii.
Dawa ya meno nime stop.
Naswaki kwa mswaki bila Dawa.

🙏🙏
 
Kikohozi kiliisha mkuu.

Nilituma Dawa Coffnil kilipona kwa siku Mbili tu.

Sina TB mkuu.
Bora ukose mali upate akili. Wewe umepata kikohozi, dawa za vikohozi ziko kibaoooo. Badala ya kununua dawa ukaanza kujitundika mitangawizi na milimao...ikasababisha vidonda kurudi.

Sasa unaendelea kujitundika mavitu, leo hiki kesho kila sijaona mahali popote umesema umeenda hospitali.

Ndugu, nenda hospital inawezekana una changamoto nyingine zaidi ya vidonda.
 
Ni kweli mkuu na Mimi nilijutia sana Kwa maamuzi yangu.

Nilikwenda Muhimbili Baada ya MATATIZO ya Tumbo.

Ilaa niliambiwa Tangawizi ni NonSteroidal Anti-Inflammatory Drugs (NSAIDs)
 
Bora ukose mali upate akili. Wewe umepata kikohozi, dawa za vikohozi ziko kibaoooo. Badala ya kununua dawa ukaanza kujitundika mitangawizi na milimao...ikasababisha vidonda kurudi.

Sasa unaendelea kujitundika mavitu, leo hiki kesho kila sijaona mahali popote umesema umeenda hospitali.

Ndugu, nenda hospital inawezekana una changamoto nyingine zaidi ya vidonda.
Akina sisi inapokuja suala la kwenda hospital sijui tunaingiaga ubarid gani,
 
Back
Top Bottom