Naomba kufahamishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba kufahamishwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Masauni, Sep 3, 2010.

 1. M

  Masauni JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikijiuliza sana, pamoja na ufisadi mkubwa uliofanywa na kikwete na CCM kwa ujumla ambao hakuna mtanzania yeyote anayeweza kupinga ,maana kila kitu kiko wazi na hata CCM wanakili kufanya ufisadi huo!!. Kwa nini basi bado kuna watanzania wanamshabikia kikwete??, Tena nasikia huko kusini wamehaidi kumpa kura nyingi tu!!
  Naomba nieleweshwe mambo yafuatayo
  Je, wananchi hawataki kuamini ufisadi uliofanywa na viongozi wao , ambao viongozi wao wamekiri kufanya ufisadi huo?
  Je, ni ile dhana ya kusema kwamba wananchi walipo kuwa wanasema ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA CCM, ni sawa na kuweka agano na miungu ya CCM? kwamba chochote watakachosema viongozi wa CCM kiwe kibaya ,kizuri fikra zao zidumu ni kweli?
  Je, ni kwamba watanzania, hawajali maisha yao , ya watoto wao, ya wajukuu wao? ndo maana hawaoni umuhimu wa kuchagua viongozi wazuri na wenye nia njema na nchi yao?
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndiyo hali halisi ya TZ, Mungu ibariki TZ....Mungu ibariki Afrika!
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kidogo umekuwa tofauti na Augustees, in short waTz wengi wamekuwa brainwashed kiasi cha kutoona mbali na kuamini kuwa bila ccm maisha bongo hayawezekani wakati maisha bora kwa kila mtz yatapatikana bila CCM!
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I will repeat here again and again -- that ours ia a country teeming with herds of sheep for humans!!!
   
 5. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii ndio BONGO au UDONGO?, wala sio UDONGO ni tope ilioza !! kweli nashindwa kufahamu ndani ya vichwa vya hawa wana NJI hii ndani kuna nini. Tanzania itajengwa na wenye moyo na italiwa na wenye meno. Chukua Chako Mapema mbele kwa mbele.
   
 6. m

  matambo JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hili ndilo tatizo kubwa walilonalo watanzania, binafsi naunga mkono mageuzi sana tu lakini hali ilivyo mikoani haitii moyo hata kidogo,
  ndio maana mie huwa nasoma na kubaki kusikitika ninapoona post za watu walioko dar es salaam wasiojua hali ya ufahamu wa watu mikoani kisha wanakuwa wabishi kuambiwa kuwa si rahisi kuitoa ccm mwaka huu kisha wanakuwa wabishi ,wakali na wenye majibu ya jeuri,

  kwa kweli uelewa wa watu ni mdogo mno mno, binafsi huwa naenda vijijini umbali wa km 200 toka makao makuu ya wilaya na mahali ambako hakuna zahanati,barabara,umeme wala maji na wananchi huko hawaelewi lolote juu ya upinzani, wao ni ccm ,ccm na kikwete tu, sababu?hawajaelimishwa!!1
  binafsi nilikuwa namuunga sana mkono marehemu chacha wangwe aliyekuwa akipendekeza kuwa chadema ielekeze nguvu mikoani na vijijini,watu hawakumwelewa lakini ndo ukweli, kama tuna nina nia ya kuiondoa ccm, hakuna haja ya kukonsetreti mijini,huko hakuna faida kwani watu tayari wamesikia mengi juu ya ccm na ufisadi na kama wanaichukia wanaichukia na kama wataipigia kwa kuwa wanaipenda basi wanaipenda tu lakini vijijini huko kusiko na barabara,zahanati,maji na umeme, huko ndiko kwa kuanzia maana watu hawa wana kero nyingi lakini hawana ufahamu while watu wa mijijini wana shida lakini si kama za vijijini

  kupita na helikopta na kufanya mkutano wa saa moja kisha unaondoka tena makao makuu ya wilaya au makao ya kata chache ndani ya wilaya kisha huachi msingi imara wa chama kijijini,katani wala wilayani kwa kweli hakutusaidii kabisa, tuige ccm yenye mfumo bora kuanzia balozi wa nyumba 10.kisha tawi ,kata,na kuendelea, huo ndio mfumo unaoonyesha uimara na uhai wa chama, kisha weka misingi namna wale viongozi wanaobaki kijijini wanaendelea kuelimisha wananchi juu ya sera za vyama pinzani
   
 7. D

  Dopas JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hilo ndilo tatizo la watanzania wengi. Hudhani kuipinga ccm ni kutenda dhambi. Ni bahati mbaya wengine huipinga bila kujua wanachofanya, hadi watakapotumbukia shimoni. Bado kuna kazi kweli. Ni mwaliko kwetu sote kuwaelimisha wapiga kura wengi kadiri tuwezavyo ili waone hitaji la mabadiliko. Haidhuru kama tutafanya makosa. Tusiogope kuthubutu kujaribu.
   
 8. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni ELIMU. Sehemu ambako kuna ahueni ya ELIMU wanaelewa kinachoendelea na wataichagua CHADEMA. Huko Kusini ELIMU bado sana.

  Hata hivyo, naamini Watanzania waelewa ni wengi kiasi kwamba CCM itawekwa pembeni wakati huu.

  Mbona Zanzibar waliweza kuidharau CCM? Hilo linawezekana Tanzania bara vile vile.

  My considered opinion is that JK will lose to Dr. Slaa. Ila Dr. Slaa asikubali kampeni itoke kwenye UFISADI. Makamba anajaribu kuitoa huko lakini amegeuziwa kibao. Kila kukicha CHADEMA izungumzie UFISADI wa vigogo wa CCM.
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kila siku nasema Watanzania ni sikio la kufa, halisikii dawa.
   
 10. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  naona unataja kusini lakini utakuja kushangaa CCM watapata kura nyingi zaidi hapahapa dar. mengi yameshaongelewa humu JF
  1. nafikiri wananchi wanajua kwa kiasi tatizo la ufisadi lakini watalink vipi na maisha yao ya kila siku huenda ndiyo hapo kuna shida
  2. mbadala wa CCM pia ni tatizo, hivi vyama siku za kawaida vinakuwepo tu DSM na kutoa matamko mbalimbali, wakati wa uchaguzi ndiyo sasa vinaenda mikoani. hivyo vinakuwa havifahamiki sana na wananchi kiasi kwamba haviaminiwi.
  3. pia kuna matatizo katika kujipanga wakati wa uchaguzi. tumeshuhudia kuwa vyama vingi ni kama vimeamka toka usingizini (hasa huko mikoani). hapa ni katika uteuzi wa wagombea nafasi mbalimbali. sasa kunakuwa na minong'ono kama baadhi ya wabunge walikuwa ma DJ, mara walikuwa bongoflava, mara ooh mgombea mwenza ni darasa la saba (CUF wamesema ni MEMKWA)nk, hawa watabadilisha nini? sasa hata watu wenye nia njema wanaona kupigia upinzani ni kurudisha matatizo yaleyale na afadhali waliopo tunawajua
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Tope linaoza?
   
 12. B

  Bull JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamekosa chama Mbadala, bora waendelee na CCM ambayo Kikwete ameahidi kupambana na ufisadi, kwani historia inaonyesha kuwa CCM wanajirekebisha mwaka hadi mwaka, chini ya uongozi wa Kikwete nchi inaweza fika mbali

  Chadema hakiwezi kuwa chama mbadala kwa sababu ni chama kinaendeshwa kwa udini na ukabila na viongozi wake wote hawana elimu inayo tambulika, mfano:

  M/Kiti Mbowe O Level
  Mgombea Mweza drasa la saba
  Mchungaji Slaaa kasomea bibilia

  Kweli hawa ni watu wa kuwakabidhi nchi ? you must be kidding!!!
   
 13. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  Bull bora uwaambie wewe! ..... Bado hamna chama cha maana kitakachoweza kufanya replacement, watanzania wakifanya makosa ya kuchaguwa chama cha upinzani basi miaka 5 ya kwanza kodi zao zitatumika kukiweka chama sawa, miaka inayofuata mtaona katika zinaazwa kabadilishwa hatimaye mtu anakaa madarakani hadi afe! washaanza kupiga kelele ubadilishaji wa katiba
   
 14. M

  Masauni JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Elimu ya kutambulika ni elimu gani?,unafahamu elimu ya makamba? Kikwete atapambana vipi wakati yeye alifanya ufisadi. Pia elimu si kigezo, raisi Zuma hakwenda shule lakini ni kiongozi mzuri, Uongozi ni talents, si kusoma. Pia kaa uelewe chini ya uongozi wa CCM ufisadi hautapunguzwa. 'top layer' yote inanuka kwa rushwa, nani atamuwajibisha mwenzake? Usijidanganye.
   
Loading...