Naomba kufahamishwa kuhusu Scholarship ya Algeria kutoka TCU

Hannat15

Member
Jul 6, 2016
33
16
Kwa anaefahamu ile scholarship ya Algeria kwenye website ya TCU naomba kufaham ile course ya english language unaenda kusoma nini celew unaenda kusoma english kivipi au unaenda kusoma english ukimlza masomo unagraduate km mwalimu wa english? Msaada wakuu.
 
miaka ya nyuma loan board walikuwa wanatoa mpaka $4500 kwa international students under bilateral agreement, mwaka huu ipo $1500 tu, soma heslb guidelines so karibu 90% utajitegemea,
 
miaka ya nyuma loan board walikuwa wanatoa mpaka $4500 kwa international students under bilateral agreement, mwaka huu ipo $1500 tu, soma heslb guidelines so karibu 90% utajitegemea,
e20f50e48d35a2e8da11736472280108.jpg
angalia apo
 
*TAARIFA MUHIMU KWA WANAFUNZI WA KITANZANIA WANAOTARAJIA KUOMBA SCHOLARSHIP YA ALGERIA*
Ndugu watanzania wenzangu, hivi karibuni lilitolewa tangazo kuhusu maombi ya scholarship ya Algeria kwa ngazi ya shahada ambapo maombi yake yatapelekwa kupitia *TCU*.
Madhumuni ya kuandika taarifa hii kutoa *_tahadhari_*kwa wale wanafunzi wanaotarajia kuomba scholarship hii. Tukiangalia mwisho wa tangazo pameandikwa:
" *This is a full scholarship hence all beneficiaries will not be receiving any loan from the Higher Education Students' Loan Board* "
Jambo la msingi ambalo nahitaji kulisema ni kwamba scholarship inayotolewa na serikali ya Algeria imejumuisha mambo yafuatayo:
*Makaazi (unapewa chumba watu 2, kitanda, godoro na shuka moja tu)
*Chakula (kwa jamii ya kitanzania wingi wa vyakula hivyo ni tofauti na ambavyo wengi wao hawawezi kula). Hata hivyo, chakula hiki hakitolewi kipindi cha likizo hata za wiki mbili mbili. Muda wote wa likizo kwa vyuo vya Algeria ni miezi minne.
*usafiri kwa ajili ya kwenda na kurudi chuo tu (na si kwengineko) tena ni usafiri wa ratiba maalum. Usafiri huu hudumu nyakati za chuo tu na hautolewi kipindi cha likizo.
*Pesa kwa mwaka ni 15,000DZD ambayo ni sawa na Tsh.300,000. Pesa hii kuipata inahitajika uwe umeshakusanya documents nyingi ambazo baadhi yao huchelewa kupatikana. Hivyo kwa wanafunzi wanaoingia mwaka wa kwanza hawawezi kuzipata pesa hizi punde wanapoingia. Inaweza kuchukua hadi mwaka kukamilisha taratibu na vigezo vya kupatikana kwa pesa hizo. Cha kuongezea ni kua pesa hii unayopewa haitoshelezi hata kwa kutumia kutoa nakala za vitu mbali mbali kwa mwaka mzima. Hii ni pesa ndogo sana kwa sababu kwa matumizi ya stationeries tu, mwanafunzi anahitaji awe na angalau 35,000DZD kwa mwaka.
Sasa naomba nitoe maelezo yafuatayo:
Matumizi mengineyo ambayo ni muhimu sana nchini ni lazima mtu ajitegemee mwenyewe 100%. Serikali ya Algeria hapa haitahusika na kumpatia mtu huduma nyengine yoyote. Huduma nyingi nchini Algeria ni ghali kuliko hapa Tanzania. Nitatoa mfano wa huduma za lazima kwa mwanafunzi:
*chakula kwa siku za likizo (ambacho hutopatiwa na ni lazima ujitegemee), pia muda masomo nyakati za mchana ukiwa class huwezi kupata kula kwa sababu chakula hutolewa muda maalum tu. Pia chakula kinatolewa kwa foleni (hostel nzima) ambayo inaweza kuchukua hadi watu 1,000. Foleni mara nyingi hua ni moja tu. Pia chakula mara nyingi hua ni kibaya mno kitu ambacho hupelekea kufanyika kwa migomo baadhi ya siku kutokana na ubaya wake hivyo hukulazimu kutafuta means nyengine kwa ajili ya kula. Wanafunzi wengi hujipikia wenyewe na chakula ni ghali mno. Mtu kwa mlo mmoja tu (mfano mlo wa mchana) anaweza akatumia takriban 350DZD sawa na Tsh.7,000.
*mavazi ujitegemee na ni ghali sana. Mavazi huvaliwa kulingana na misimu ya joto na baridi kali. Nitataja mavazi ya kiume yenye bei nafuu kabisa. Suruali jeans @4,000DZD=Tsh80,000. Tshirt nzito @3,000DZD=Tsh60,000. Koti la baridi @6,000DZD=Tsh120,000. Suruali nyepesi @3,000DZD, shati nyepesi @2,500DZD, viatu @6,000DZD. Hapo cjata mavazi ya ndani. Mavazi ya kike ni ghali zaidi.
*usafiri kwa safari zisizo za chuo ujitegemee. Daladala ni 20DZD kwa direction. Kwa safari ambazo daladala haifiki ni lazima uchukue taxi na nauli ni 350DZD kwa masafa ya wastani.
*matumizi ya internet na mawasiliano ni ghali sana. Angalau yote kwa pamoja uwe na 5,000DZD kwa mwezi.
*Ukifika Algeria ni lazima utengezewe Residence permit. Nayo ni lazima uilipie angalau 8000DZD kwa process zote hadi kukamilika. Zoezi hili lazima ulirudie kila baada ya miaka 2.

Kutoka na mda na shughuli nyingi, sitoyataja mambo yote hapa ila yako mengi zaidi ya hayo. Nitatoa wastani wa pesa ambazo mwanafunzi mwenyewe atalazimika kujitegemea nchi Algeria kwa mwaka. Ili mtu aweze kusurvive nchini Algeria, ni lazima awe na angalau *6,000USD* kwa mwaka. Hapo ataweza kutumia kwa kujibanabana na atasurvive.

Tanbih: hapo zamani wanafunzi walikua wakipatiwa mkopo kupitia HESLB ila sasa bodi imeamua kujitoa katika hilo. Hivyo, kutokana na maelezo niliyoyatoa hapo juu, ni lazima muombaji kwa sasa awe na uwezo wa kutosha wa kujisomesha mwenyewe. Maamuzi ya mtu kuomba scholarship hii yapo mikononi mwake. Mimi nimetoa tahadhari tu

Mimi pia ni miongoni mwa wanafunzi wanaosoma Algeria...huo ndo ukwel uliopo hadi sasa...ahsante
 
Back
Top Bottom