Naomba kufahamishwa, hilio la mtu kufariki akaacha pesa zake benki

commm

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
1,674
1,905
Wakuu kwanza kabisa nawasalimu wote. Habari za asubuhi

Okay, turudi kwenye mada.

Wakuu kuna hili suala ambalo nimekua nikijiuliza na kuuliza baadhi ya watu lakini bado sijapata majibu.

Iko hivi; endapo ikitokea mtu akafariki na kwa bahati alikua ana akiba ya fedha labda kwenye akaunti ya bank au kwenye akaunti hizi za mitandao ya simu.

Je, ni utaratibu gani ambao unatakiwa kufuatwa na ndugu wa marehemu ili kupata hizo fedha?

Nawasilisha.
 
Nafikiri pakuanzia ni mahakamani kwaajili ya kufungua mirathi, Na kama wanafamilia mumchague kabisa msimamizi wa mirathi. Baada ya hapo mahakama itawapa utaribu wote wa kufuata japo mlolongo wake ni mrefu kidogo mpaka kuja kupata.
 
Kama ni bank wakati unafungua acount si ulijaza sehemu ile ya wadhamini na namba zao za simu ukaweka?basi wale ndio wako kwenye patikula yako bank wao ndio wanawez nenda na hati yako ya kifo wakakabidhiwa mzigo uloacha na kwenye simu nadhani hadi uende mahakamani upande wamirathi
Wakuu kwanza kabisa nawasalimu wote. Habari za asubuhi

Okay, turudi kwenye mada.

Wakuu kuna hili suala ambalo nimekua nikijiuliza na kuuliza baadhi ya watu lakini bado sijapata majibu.

Iko hivi; endapo ikitokea mtu akafariki na kwa bahati alikua ana akiba ya fedha labda kwenye akaunti ya bank au kwenye akaunti hizi za mitandao ya simu.

Je, ni utaratibu gani ambao unatakiwa kufuatwa na ndugu wa marehemu ili kupata hizo fedha?

Nawasilisha.
 
hatua ni ndugu zake kwenda na hati ya kifo, na barua kutoka serikali ya mtaa kudhibitisha mwenye akaunti amefariki.
 
Wakuu kwanza kabisa nawasalimu wote. Habari za asubuhi

Okay, turudi kwenye mada.

Wakuu kuna hili suala ambalo nimekua nikijiuliza na kuuliza baadhi ya watu lakini bado sijapata majibu.

Iko hivi; endapo ikitokea mtu akafariki na kwa bahati alikua ana akiba ya fedha labda kwenye akaunti ya bank au kwenye akaunti hizi za mitandao ya simu.

Je, ni utaratibu gani ambao unatakiwa kufuatwa na ndugu wa marehemu ili kupata hizo fedha?

Nawasilisha.
Mimi pia nilikuwa na wingu juu ya swali kama lako; Ni hivi hakuna kinachoweza kupotea the system designed to favour the customer as well as the entity.

Ikitokea bahati mbaya mteja akatangulia mbele za haki ni kwamba baada ya kukaa kikao kuchagua msimamizi wa mirathi na minutes za kikao zikapelekwa mahakamani basi msimamizi wa mirathi atasimama na kufuatilia kila suala including kufuatilia kwenye mitandao ya simu na banks!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom