Jiamini kwa kufuata mambo haya 5

Gentlemen_

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
3,563
10,552
Habari zenu wakuu..
Bila kupoteza muda leo nineona nije na huu uzi kuokoa baadhi ya watu wenye (Insecurities) ambao hawajiamini na wengine wanaenda mbali zaidi hawajipendi.

So Kutojiamini kukizidi kunazaa kutojipenda, yaani unajichukia wewe mwenyewe.

Kuna makundi mengi ya watu ambao hawajiamini mfano:-

1- Kutojiamini kwa kukosa Fedha
2-Kutojiamini kwa kukosa Elimu kubwa
3-Kutojiamini kwa kukosa Mwili wenye mvuto
4-Kutojiamini kwa kuwa na changamoto za Kiafya
5-Kutojiamini katika Mahusiano.


Zifuatazo ni njia za kujiongezea kujiamini kwa kuzingatia hayo makundi niliyoyataja juu

1- Jitahidi uwe na Akiba ya pesa
:

Hakuna mtu ambaye ana hela alafu asijiamini labda uyo mtu awe na kasoro nilizoambatanisha hapo juu. Ila asilimia kubwa watu wenye hela huwa na (overconfidence) hata wakiwa ktk sehemu za starehe, kwenye Michezo na ktk matukio ya kifamilia.

Kitendo cha kuwa na Akiba ya pesa kinakupa hali ya kujiamini kwa kuwa unajua wapi pa kukimbilia ikitokea hali ya kiuchumi imezorota.

2- Jitahidi uongeze Elimu kila uchwao:

Binafsi siamini ktk elimu ya darasani kwamba itamkomboa kila mtu, bali elimu ya Mtaani ndio kila kitu. So kwa wale wenye elimu ndogo au elimu duni, wanatakiwa waongeze maarifa ya mtaani na yale maarifa mtambuka mfno kujua lugha ya biashara (English).

Kuna maneno yalivuma zamani baada ya kuona aliyekuwa kiongozi wetu wa nchi kutopenda safari za nje ya nchi watu walisema Mzee hajui lugha! So akawa na Kutojiamini.

3- Jitahidi kujiamini hatakama umekosa Mwili wenye mvuto:

Hapa ndipo hatari zaidi, kuna watu hawajiamini hasa wadada wenye maumbile flani ambayo kwa wao wanajiona ni wabaya na hawavutii hali inayopelekea kujiongezea au kujipunguzia baadhi ya vitu.

Hawa huwa hawajiamini hata akiwa na hela kiasi gani, cha msingi ni kukubali hali uliyonayo na ujue kabisa wapo watu wanapenda hivyo ulivyo mfano mimi napenda warembo wembamba akiwa mwenye kujazia sikatai ila first preference ni kimodo. So Wanaume tupo wenye mahitaji mbalimbali.

Pia kwa wanaume wafupi nao hawajiamini.. Nyie ndugu zangu mjitahidi kuwa wapole na hakika wapo wanawake wenye kupenda watu wafupi. Mtu unatakiwa kujikubali na hali yako.

4- Changamoto za Kiafya zikubali na kamwe zisikufanye usijiamini:

Kuna baadhi ya ndugu zetu wanapitia hali ngumu ya kiafya mfano:-
Kuna wenye shida ya pumu, selimundu, matatizo ya moyo, upungufu wa nguvu za kiume , Ugumba na mambo mengine. Huwa hawajiamini na wanaishi kwa tahadhari kubwa (Vizuri kufanya hivyo) ila kuna point inatakiwa ukubali hali yako na ujiamini kwamba "naweza+nitaweza+nitapona+nitaishi"

Kuna usemi wanasema kuna nguvu ya neno yaani the way ukiwa unajinenea mambo mazuri basi na kweli huwa yanatokea. Kuna baadhi ya magonjwa yanatokea kwa kutojiamini.

5- Mapenzi usiyape kipaumbele..!!

Ndio. Mapenzi yasipewe kipaumbele hasa kwa wale wenye shida ya wivu. Wivu wa kimapenzi unasababishwa na hali ya kutojiamini! Naaam.

Ukiona mtu ana wivu sana ujue hajiamini na sio kama anakupenda/anapenda sana hapana. Huyu mtu hajiamini anaona muda wowote anakosa jimbo.

Sasa nini cha kufanya? ni kuyaweka mapenzi kando, usiyape kipaumbele sana hali hii itakupunguzia wivu. Kuna watu hawajiamini kwenye mahusiano na mara nyingi aina hii ya watu ndio hufanya matukio mabaya sana. Pia aina hii ya watu ndio wale overprotective kwa wenza wao! 'Upo wapi? Upo na nani?"Upo kwenye mahusiano lakini kiuhalisia upo ktk kifungo cha mapenzi..


Mwisho kabisa:
Ningependa nimalizie kwa kuongeza hii (trick).


Jitahidi unukie vizuri, hii kitu muhimu sanaaa! Binafsi nimeifanyia tafiti kwa muda mrefu nimeona siku nikipiga unyunyu wangu fresh najiona nimejiongezea kujiamini kupita maelezo.

1- kila sehemu ukipita akili inakwambia nimeacha balaa huko

2- Kila ukipishana na mtu especially mrembo unajua kbs huyu bidada kapishana na hewa maridhawa...

3- Ofisini kwenye makorido ukipishana na mtu lazima aweke heshima.. Sometimes unaulizwa 'Bro unatumia perfume ipi!"

4- Ni kawaida kuombwa namba ya simu na mrembo (Hili nalo mkalitizame).

5- Hizi vitu ni seduction tosha.. Hutongozi. Na ikitokea umetongoza basi huongei saana mtoto analala kifuani mwenyewe.


Hasara:!!
1- Utambulisho: Wanajua flani alikuwepo hapa, yupo, au yupo maeneo ya hapa!..

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom