Naomba kufahamishwa gharama ya Kujenga msingi

olele

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
1,303
1,559
Habari zenu wakuu, nilitaka kuanza ujenzi ila kwa awamu, sasa nimemuuliza mchora ramani (kuna ramani nataka kuichukua kutoka kwake) vyumba ni vitatu (master included) nikamuuliza msingi wake unaweza kugharimu bei gani?

kaniambia mil 12 kidogo nizimie.

Ambao mmejenga naombeni mnijuze mlitimia sh ngapi kwenye msingi.
 
Habari zenu wakuu, nilitaka kuanza ujenzi ila kwa awamu, sasa nimemuuliza mchora ramani (kuna ramani nataka kuichukua kutoka kwake) vyumba ni vitatu (master included) nikamuuliza msingi wake unaweza kugharimu bei gani?
kaniambia mil 12,
kidogo nizimie...

ambao mmejenga naombeni mnijuze mlitimia sh ngapi kwenye msingi
Na hapo bajeti yako unakuta ilikuwa milioni 5.
 
Inategemeana inaweza kufika au ikazidi inategemea unajenga msingi wa aina gani wa kumwaga zege au bila zege, inategemea kiwanja kipo eneo gani tambarale au bondeni
Gharama zinategemeana na na size ya nyumba, Layout ya kiwanja na asili ya udongo wa hapo unapojenga.
 
Habari zenu wakuu, nilitaka kuanza ujenzi ila kwa awamu, sasa nimemuuliza mchora ramani (kuna ramani nataka kuichukua kutoka kwake) vyumba ni vitatu (master included) nikamuuliza msingi wake unaweza kugharimu bei gani...
Kama unajenga kule olele hiyo ndiyo gharama yake. Nunua materials yote , tafuta fundi mpe Sh 300 kwa tofali
 
Habari zenu wakuu, nilitaka kuanza ujenzi ila kwa awamu, sasa nimemuuliza mchora ramani (kuna ramani nataka kuichukua kutoka kwake) vyumba ni vitatu (master included) nikamuuliza msingi wake unaweza kugharimu bei gani..
Aiseee hiyo hela ni mingii.. nmejenga msingi juzi tu kwa 4.9M, nyumba vyumba 3, viwili self-cointained, sebule, dining, kitchen na parking... Wasikutishee..
 
Amekiona kiwanja mpaka akafikia kusema hiyo bei? Kama hajakiona kiwanja basi huyo ni murongoooo labda iwe msingi wako ni mkubwa sana vyumba vipana.

Binafsi ninadhani yupo sahihi kwa sababu huenda hapo amejumlisha na gharama za rough floor ya zege yenye kokoto zile nyeusi ngumu, lazima ifike hata milioni 9 kwa nyumba ya vyumba vitatu vya kulala, sebule, dining, jiko, verandah na vyoo na pengine kuna vikorido.

Wewe unachotakiwa kufanya si kukata tamaa ama kuona hela aliyotaja ni kubwa, wewe anza na ulichonacho mkononi muda huu, mambo huwa yanajiseti unavyoona kazi inafanyika unapata tu hela na unapata kasi. Go bro!
 
Habari zenu wakuu, nilitaka kuanza ujenzi ila kwa awamu, sasa nimemuuliza mchora ramani (kuna ramani nataka kuichukua kutoka kwake) vyumba ni vitatu (master included) nikamuuliza msingi wake unaweza kugharimu bei gani...
Gharama ya msingi inategemea uko wapi, ardhi mutakapojenga. Ukiwa Dar simenti bei choni lakini msingi una gharama. Ukiwa mikoa ambayo simenti ni sh 21,000 hapo unaona utakavyolika. Msingi unaweza kuwa kati ya million 8-12.
 
duh asante sana mkuu, umenipa mwanga
Hii hapa budget yangu Vs Actual.. tena hapo cement nimepigwaa.. 15,000/ mpaka site sio 16,000/
1630911640325.png

Nenda kajenge kakaa, wasikukatishe tamaa... narudia tena.. nenda kajenge kijana mwenzanguuu.. na Mungu akutie nguvu kwenye hilo..
 
Hii hapa budget yangu Vs Actual.. tena hapo cement nimepigwaa.. 15,000/ mpaka site sio 16,000/
View attachment 1926030

Nenda kajenge kakaa, wasikukatishe tamaa... narudia tena.. nenda kajenge kijana mwenzanguuu.. na Mungu akutie nguvu kwenye hilo..
Wengi wanaficha ukweli. Ilimradi tu wakukatishe tamaa. Asante mkuu.

Mi nyumba nayoifikiria kujenga ni 13× 12. Vyumba 3, kimoja masta, sebule, dining, na public toilet. Nafikiri hii bajet itanifaa sana japo kiwanja kina slope kidogo.
 
Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom