Naomba kueleweshwa mfumo wa trade test (VETA)

Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
11,045
15,380
Wakuu mwenye uelewa na mfumo huu naomba aweke wazi. Maana kuna mkanganyiko mkubwa sababu veta wanatumia Levels na grades.

Kama kuna mtu anajua equivalents za levels na grades vizuri atuambie
 
Mfumo wa grades ulikuwa ni wa zamani na ulikuwa hauna mwendelezo ikiwa utafika grd one ambayo ni equivalent to level 3 nowadays, lakini hivi sasa kuna Mfumo wa CBA ambao unatoa certificate in levels, mwanachuo anayo nafasi ya kuendelea na level 4,kwan kuna masomo ambayo yameongezwa ktk Mfumo huu kama vile technical drawing, engineering science, entrepreneur, Engl & comm skills, life skills pamoja na fani husika.
Mfano mwanachuo wa umeme ni lazima kusoma masomo hayo ili kuwa na nafasi ya kuendelea na level zingine. Hii ni tofauti na hapo zamani ambapo alisoma fani husika tu na kuifanyia mtihani wa theory na practical.
Madaraja kwa sasa n VC 1=level 1 =grd 3, VC 2 =level 2 =grd 2 na VC3 =level 3=grd 1. Naomba kuwasilisha
 
Mkuu sorry na vipi kuhusu vyeti vya veta. Kozi zipi zinpaswa kusoma masomo hayo yaliyoongezwa?
 
Cheti kipya cha VETA CBA
e222136b4af04fd10d9c9eb013f6f031.jpg
 
Cheti kipya cha VETA CBA
e222136b4af04fd10d9c9eb013f6f031.jpg
Bro vp ninampango wa kusomea mechanical engineering hapo baadae hivyo nilikuwa naomba kujua kama nikishapata cheti cha CBA level 2 nitaweza kujiunga na vyuo kama ATC na DIT kufanya pre-technology program na kuendelea na ordinary diploma
 
Hapo inakupasa uendelee na level 3, ukimaliza ndio utaweza kuendelea na Diploma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika mkuu. Ukifanya pre technology programs zina kuruhusu kuendelea na diploma ukiwa na (CSEE) na (NVA) Level III
Mkuu nisaidie. Kuna kijana amemaliza form4 arts na amepata D nne katika masomo 7. Tumeangalia mahitaji ya college wengi wanasema D4 zinahitajika. Issue kama ushindani ni mkubwa kuna uwezekano wa kukosa, nilitaka nimshauri aangalie VETA pia lakini sijajua akienda VETA ana anzia na level Gani? Tunafikiria courses kama ICT.
 
Kwa VETA ushindani ni mkubwa zaidi, sababu ya unafuu wa gharama. Inabidi aanze Level 1, kwa fani ya TEHAMA inatolewa KIPAWA ICT CENTER na DSM RVTSC (VETA CHANG'OMBE)
 
Kwa VETA ushindani ni mkubwa zaidi, sababu ya unafuu wa gharama. Inabidi aanze Level 1, kwa fani ya TEHAMA inatolewa KIPAWA ICT CENTER na DSM RVTSC (VETA CHANG'OMBE)
Ahsante. Hizi levels za VETA kila moja huchukua muda gani kumaliza?
 
Back
Top Bottom