Naomba kuelekezwa kusoma mita za maji

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
685
484
Ndugu wanaJF,

Ninaomba mwenye ujuzi wa kusoma mita za maji anijuze.

Yangu imeandika 13 mita za ujazo! Hivi gharama kwa mita moja ya ujazo ni shilingi ngapi?

NINAOMBA MSAADA WENU WADAU
 
Kwanza muulize anayekuuzia maji anakuuzia mita moja kwa tsh ngapi? Kisha tutakusaidia kuzidisha kwa hiyo 13
 
Kwanza muulize anayekuuzia maji anakuuzia mita moja kwa tsh ngapi? Kisha tutakusaidia kuzidisha kwa hiyo 13
Maji ni ya mamlaka ya maji mkoani hapa, lengo la kuuliza ni kwamba mwezi uliopita sikupewa bill nilipokwenda kuidai ili nilipie wakadai msomaji wao bado hajapeleka ofisini alichosoma kwenye mita!Hadi sasa bado sijaletewa bill.
 
Maji ni ya mamlaka ya maji mkoani hapa,lengo la kuuliza ni kwamba mwezi uliopita sikupewa bill nilipokwenda kuidai ili nilipie wakadai msomaji wao bado hajapeleka ofisini alichosoma kwenye mita! Hadi sasa bado sijaletewa bill.
Unit moja ni 1650, sasa hapa ni ngumu kujua kama hizo unit 13 ni toka uanze kutumia mita au la!, maana mfano saa hivi ikisoma 13 mwezi ujao ikasoma 19 utachukua 19-13 utapata 6 ina maana umetumia unit 6 na 6 mara 1650 jawabu utakalopata ndilo deni.
 
unit moja ni 1650, sasa hapa ni ngumu kujua kama hizo unit 13 ni toka uanze kutumia mita au laha maana mfano saa hivi ikisoma 13 mwezi ujao ikasoma 19 utachukua 19-13 utapata 6 ina maana umetumia unit 6 na 6 mara 1650 jawabu utakalopata ndilo deni.
Mita ni mpya, namaanisha ni eneo jipya kuwekewa maji. Ndiyo maana hata nilipokwenda walidai msomaji hajaleta bill za maunganisho mapya!
 
Maji ni ya mamlaka ya maji mkoani hapa,lengo la kuuliza ni kwamba mwezi uliopita sikupewa bill nilipokwenda kuidai ili nilipie wakadai msomaji wao bado hajapeleka ofisini alichosoma kwenye mita!Hadi sasa bado sijaletewa bill

Tulia hadi siku wakikuletea bill hata ikiwa kubwa utailipa kidogo kidogo kwa kadri utakavyoweza kwasababu sio kosa lako ni lao.
 
Tulia hadi siku wakikuletea bill hata ikiwa kubwa utailipa kidogo kidogo kwa kadri utakavyoweza kwasababu sio kosa lako ni lao.
Asante kwa ushauri!Nimekuja hapa jukwaani kwa sababu nilipokwenda waliniambia kuwa kwa kuwa ni maunganisho mapya niende kwenye ofisi moja pale wanitengenezee control number ambayo niliweka sh.5000/ Kama kianzio wakidai ni kwa muda huu bado nasubiria bill
 
Mkuu kua makini inawezekana hiyo 5000 wamekupiga maana control namba haitengenezwi kwenye ofisi ya mtu bali inakuja pamoja na bill, na kila bill ina control namba tofauti.
 
Ndugu wanaJF,

Ninaomba mwenye ujuzi wa kusoma mita za maji anijuze. Yangu imeandika 13 mita za ujazo! Hivi gharama kwa mita moja ya ujazo ni shilingi ngapi?

NINAOMBA MSAADA WENU WADAU
[/QU
Kusoma mita rahisi tu inaaanza na masifuri 00000, 00001 na kuendelea.​
Kwahiyo uwe unaangalia siku anayokuja msoma mita unaangalia unaweka kwenye kumbukumbu.
Mfano mwezi huu namba zikasoma 00020,mwezi ujao zikasoma 00031.
Unachukua 31-20= 11 Units ndiyo yatakuwa matumizi yako kwa mwezi huo.
Kumbuka mita huwa hairudi nyuma inaenda mbele tu mpaka maelfu.
Kwahiyo itagemea na mamlaka wanaauzaje kwa unit moja Kama Ni sh 600
Chukua 11XTsh 600=6600Tsh
 
Kwanza muulize anayekuuzia maji anakuuzia mita moja kwa tsh ngapi? Kisha tutakusaidia kuzidisha kwa hiyo 13
Utamsaidiaje tena wakati umemaliza kila kitu mkuu?

Yaani mwanafunzi umemuonesha majibu kisha unampatia mtihani!

Umemjibu vizuri sana ingawa kifupi, maana ungelimsomesha tena kuwa '1' kwenye mita inawakilisha unit 1 ama lita 1000.

Kila mkoa wana bei zao, aende huko 'shiuwasa' akaulize bei ya unit moja ni sh.ngapi ndiyo azidishe na alichokichabo kwenye mita yake.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Bill za maji kuanzia Mwezi wa 6 na wa 7 ni kubwa sana nadhani wanatafuta fedha za uchaguzi.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Mita ni mpya, namaanisha ni eneo jipya kuwekewa maji. Ndiyo maana hata nilipokwenda walidai msomaji hajaleta bill za maunganisho mapya!
basi zitakuwa hizo hizo units so zidisha mara 1650 utakachopata ndo den lako
 
Ndugu wanaJF,

Ninaomba mwenye ujuzi wa kusoma mita za maji anijuze.

Yangu imeandika 13 mita za ujazo! Hivi gharama kwa mita moja ya ujazo ni shilingi ngapi?

NINAOMBA MSAADA WENU WADAU
chukua 13units×1650tsh=21,450Tsh

hyo 1650 n bei ya Unit moja. japo bei znatofautiana kutokana na eneo ulilopo.
 
Utamsaidiaje tena wakati umemaliza kila kitu mkuu?

Yaani mwanafunzi umemuonesha majibu kisha unampatia mtihani!

Umemjibu vizuri sana ingawa kifupi, maana ungelimsomesha tena kuwa '1' kwenye mita inawakilisha unit 1 ama lita 1000.

Kila mkoa wana bei zao, aende huko 'shiuwasa' akaulize bei ya unit moja ni sh.ngapi ndiyo azidishe na alichokichabo kwenye mita yake.
Siwezi tena kumuelekeza
Maana ushamaliza kila kitu, kazi kwake
 
Back
Top Bottom